Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii hawajui madhara ya matumizi holela ya mitandao hiyo au hawataki kujihadhari na hatari zinazowakabili,ripoti imetolewa jana mjini Washington katika jarida la taasisi isiyo ya kiserikali, Consumer Reports Ripoti hiyo inasema watumiaji wapatao 13 milioni wa Marekani hawajui au hawataki kutumia nyenzo za kujiweka salama kwenye mtandao wa facebook.Uchunguzi unaonesha kuwa wamarekani wapatao 4.5 milioni huwa wanaandika kwenye facebook wapi watakwenda na muda gani katika siku fulani na hii ni njia mojawapo ya kuwataarifu watu wabaya wanaoweza kudhuru,na pia kuna idadi nyingine ya wamarekani 4.7 milioni ambao wame `like` page zinazohusu mambo ya afya na tiba na kutoa taarifa za afya zao,bila ya kutambua kuwa kufanya hivyo ni kuyanufaisha makampuni ya bima. Ripoti inaendelea kudokeza kuwa ni asilimia 37 tu ya watumiaji wa facebook ndio waotumia nyenzo za
Wachunguzi hao wamewashauri wamiliki wa facebook kulichukulia suala la usalama wa taarifa za watumiaji kwa umakini kwa kuweka nyenzo zitakazo dhibiti watumiaji wajanja.Pia wametahadharisha kuwa taarifa za watumiaji zinapochukuliwa ni jambo la hatari
Watumiaji walioulizwa mikakati yao katika kuweka salama taarifa zao kwenye facebook walitoa majibu ya kustaajabisha,robo yao huwa wanaweka taarifa za uongo kwenye akaunti zao za facebook,ikiwa ni pamoja na majina na tarehe za kuzaliwa
Idadi ya watu waliokiri kutumia taarifa za uongo imeongezeka maradufu ukilinganishwa na miaka miwili ilyopita swali hilo hilo lilipoulizwa,ingawa kisheria kitendo hicho ni kinyume na mkataba wa
Mtandao wa facebook umeshaingia kwenye soko la hisa kuuza hisa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 10,ikiwa ni kiasi kikubwa zaidi kuwahi kuuzwa na kampuni za internet katika soko la hisa la Wall Street Idadi ya watumiaji wa facebook duniani imeongezeka na kufikia milioni 901 hadi ilipofika robo ya mwaka kwa mujibu wa nyaraka za







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)