POLAND NA UGIRIKI NGUVU SAWA UFUNGUZI EURO 2012 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

POLAND NA UGIRIKI NGUVU SAWA UFUNGUZI EURO 2012

Mshambuliaji wa Ugiriki, Dimitris Salpingidis (kulia) akichezewa rafu na kipa wa Poland, Wojciech Szczesny usuku huu katika mechi ya ufunguzi ya Euro 2012(Picha na  Matt Dunham/AP)
 
WENYEJI washiriki wa Euro 2012 wametoka sare ya 1-1 na mabingwa wa 2004, Ugiriki usiku huu katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo, ambao timu zake zilipoteza mchezaji mmoja mmoja kwa kadi nyekundu.
Bao la kipindi cha kwanza la Robert Lewandowski liliwapa Poland fursa ya kuongoza mchezo kwa muda mfupi, kabla ya kipindi cha pili Ugiriki kupoteza mchezaji mmoja, wakati Sokratis Papastathopoulos alipoonyeshwa kadi nyekundu na refa wa Hispania, Carlos Velasco Carballo.
Pamoja na hayo, Dimitris Salpingidis - aliyeingia mwanzoni mwa kipindi cha pili alisawazisha dakika ya 51.
Poland ilinusurika kufungwa wakati Wojciech Szczesny alipotolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumuangusha Salpingidis na kusababisha penalti, lakini kipa aliyechukua nafasi yake,Pzremyslaw Tytonsaved aliokoa penalti ya Nahodha, Giorgos Karagounis.
Mechi nyingine ya Kundi A kati ya Urusi na Jamhuri ya Czech Republic itachezwa baadaye mjini Wroclaw, Poland.
Poland wanashirikiana na Ukraine, kuandaa fainali hizi, ambao watacheza na Sweden mechi yao ya ufunguzi Jumatatu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages