Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akizindua rasmi mradi wa
uvunaji maji ya mvua uliopo Hospitali ya Wilaya ya Iringa iliyopo
Frelimo mjini hapa jana. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya
Serengeti (SBL) na kugharimu zaidi ya Shilingi Milioni 50 na unataraji
kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo zaidi ya 100,000. Wengine kutoka
kushoto ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi, Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,
Afya na Elimu, V Mushi.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akimshukuru Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda kwa
kampuni yake kufadhili mradi huo muhimu wa maji Hospitalini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akifungua maji kutoka katika tanki moja wapo.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akimtwisha ndoo ya Maji
Augusta Mtemi ambaye ni Diwani wa Viti Maalum Iringa ikiwa ni ishara ya
uzinduzi huo.
Diwani Augusta Mtemi akifurahia zoezi hilo.
Matanki ya maji makubwa yaliyowekwa ardhini katika mradi huo
Tanki litakalo tumika kusambaza maji katika mradi huo.
Hii ndio Hopspitali ya Frelimo iliyopo Manipaa ya Iringa ambayo itafaidika na mradi huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)