Kampuni
ya bia ya Serengeti imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali hapa
nchini kukabidhi zawadi kwa washindi wa zawadi hizo katika promosheni
inyoendelea’VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL, inayoendeshwa na
kampuni hiyo kwa kipindi cha wiki 7 sasa na kubakisha takribani wiki 9
ili kuisha kwa promosheni hiyo ya kipekee kabisa kutokea hapa nchini
Tanzania hakika watanzania wengi wananufaika na kupiga hatua mbele kimaisha.A
Asubuhi
ya leo droo ya nne katika promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA
KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL
zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kuhudhuriwa na waandishi wa
habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka
ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati
Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House
Coopers.
Kampuni
ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti premium
Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni hiyo nchi
nzima ambapo kwa mara nyingine wikim iliopita wadau,washiriki na
watanzania wote walishuhudia washindi wa bajaj na pikipiki wakikabidhiwa
zawadi zao huko mafinga na Iringa mjini mkoani Iringa.Mshindi wa
mafinga aliwa bw. Fadhili Manzi aliyejishindia bajaj mpya, kutoka iringa
mjini ni bw. Octavian Chagula ayeibuka na pikipiki mpya kabisa.
Akionge
na wandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo hiyo, meneja wa bia ya
serengeti lager bw. Allan Chonjo amesema lengo hasa la promosheni hiyo
ni kujaribu kusaidia jamii kwa njia ya bahati na nasibu ili kuwafikia
watanzania wengi zaidi bila upendeleo.
“
Bado tunaendelea kuwahamasisha wateja wetu na watanzania wote wenye
umri unaruhusu kushiriki katika promosheni hii waendelee kushiriki bila
kukata tamaa kwani bado kuna zawadi nyingi sana hadi zifikie milioni
780.
Washindi
wetu katika droo hii ya saba ni Salvatory Herald 52 kutoka Tanga na
Leonard Mkumbwa kutoka Dar es Salaam ambao wote kwapamoja wamejishindia
jenereta, na Jacob Mgendi 27 kutoka Mwanza ambaye amejinyakulia bajaj
mpya huku Mbaraka Adam32 kutoka kiwalani jijini Dar es Salaam akiibuka
na pikipiki mpya kabisa zawadi zote kutoka SBL ambapo kwa mara ya tatu
mfululizo, washindi wa bajaj wamekuwa wakipatikana Mwanza na kufikisha
idadi ya bajaj 3 kutoka SBL mkoani mwanza.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)