Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akimkaribisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt.
Sulaiman Al Fahim wakati walipokutana leo, Jumamosi, Juni 2, 2012, Ikulu Dar es
Salaam. Dkt. Al Fahim ambaye ni mwenyekiti wa zamani na mmiliki mwenza wa Klabu
ya soka ya Portsmouth ya Uingereza yuko nchini kuangalia uwezekano wa kuwekeza
katika uchumi wa Tanzania. Dkt. Al Fahim pia ndiye aliyeongoza mazungumzo na
kununuliwa kwa klabu bingwa ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Manchester City na
Kampuni ya Arabuni.
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika mzungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt.
Sulaiman Al Fahim
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt.
Sulaiman Al Fahim mara baada ya mazungumzo yao Ikulu leo. (Picha na fredy Maro).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)