Meneja wa kitengo cha uchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Mwanaidi Mahiza akitoa elimu ya uhifadhi
na utunzaji wa karatasi za madodoso ya Sensa ya watu na makazi 2012
kwa waratibu wa Sensa kutoka mikoa na wilaya zote nchini katika mafunzo
ya awali yanayoendelea mjini Morogoro.
Waratibu wa Sensa ya watu na Makazi 2012 kutoka katika mikoa na wilaya
zote nchini wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu mjini Morogoro. Katika mkutano huo wa mafunzo mambo
mbalimbali yanajadiliwa yakiwemo masuala ya Bajeti, Ushiriki wa
Viongozi katika Zozi la Sensa, Utunzaji na ujazaji wa madodoso wakati
wa Sensa, namna ya kuwapata makarani wa Sensa na vitendea kazi.
Viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bara na ile ya Mtakwimu mkuu
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,viongozi wa mkoa wa Morogoro na
waratibu wa Sensa ya watu na makazi 2012 wakiwa katika picha ya pamoja
na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa Bw. Alphayo Kidata (mstari wa kwanza katikati)mjini Morogoro.
Waratibu wa Sensa ya watu na makazi wakipitia moja ya dodoso
litakalotumika wakati wa Sensa ya watu na makazi mwezi Agosti mwaka
huu na kujifunza namna sahihi ya kuweka vivuli/ alama wakati wa
kukusanya taarifa za kaya.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)