Meneja
wa kitengo cha uchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bi. Mwanaidi Mahiza, akitoa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa
karatasi za madodoso ya Sensa ya watu na makazi 2012 kwa waratibu wa
Sensa kutoka mikoa na wilaya zote za nchini wakati wa mafunzo ya awali
yanayoendelea mjini Morogoro.
Waratibu
wa Sensa ya watu na Makazi 2012 kutoka katika mikoa na wilaya zote
nchini wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu mjini Morogoro, wakati wa mkutano huo wa mafunzo,
ambapo mambo mbalimbali yanajadiliwa yakiwemo masuala ya Bajeti,
Ushiriki wa Viongozi katika Zozi la Sensa, Utunzaji na ujazaji wa
madodoso wakati wa Sensa, namna ya kuwapata makarani wa Sensa na
vitendea kazi.
Viongozi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bara na ile ya Mtakwimu mkuu wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,viongozi wa mkoa wa Morogoro na waratibu
wa Sensa ya watu na makazi 2012 wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Bw. Alphayo Kidata (mstari wa kwanza katikati) mjini Morogoro.
Waratibu
wa Sensa ya watu na makazi wakipitia moja ya dodoso litakalotumika
wakati wa Sensa ya watu na makazi mwezi Agosti mwaka huu na kujifunza
namna sahihi ya kuweka vivuli/ alama wakati wa kukusanya taarifa za
kaya. Picha Zote na Aron Msigwa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)