Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed
Ali, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa
mazungumzo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Mhe. Amour Zacarias
Kupela, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo
kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake nchini.
***************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMKARIBISHA BALOZI WA SUDAN NCHINI NA KUMUAGA WA MSUMBIJI, IKULU JUNI 05, 2012
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
leo Jumanne ya Tarehe 05 Juni 2012 amekutana na Mabalozi wa nchi za
Sudan na Msumbiji waliomtembelea ofisini kake Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Balozi
wa kwanza kufika alikuwa Balozi wa Sudan nchini Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Yassir Mohamed Ali ambaye amekutana na Makamu wa Rais kwa mara ya
kwanza na katika kujitambulisha kwake akaelezea nafasi ya Tanzania
katika kuhakikisha Bara la Afrika linabakia kuwa na amani na utulivu.
Balozi
Mohammed alimwambia Makamu wa Rais kuwa wafanyabiashara kutoka Sudan
wamekuwa wakishiriki katika uwekezaji nchini na bado wapo ambao wana nia
ya kufanya hivyo na kwa kuanzia wafanyabiashara hao watashiriki katika
maonyesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Saba Saba
yatakayofanyika mwaka huu.
Balozi
huyo alieleza pia kuwa, Sudan inadumisha uhusiano wake na Tanzania
katika kuhakikisha nchi mbili zinabakia kuwa na lengo moja kubwa la
kuwapatia wananchi maendeleo.
Kwa
upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais, yeye alimkaribisha Balozi
Mohammed na kumwahidi kuwa Tanzania itazidi kutumia nafasi yake katika
kuhamasisha amani hasa sasa ambapo nchi ya Sudan iko katika mgogoro na
Sudan ya Kusini.
Balozi
Amour Zacarias Kupela wa Msumbiji, yeye sambamba na kumuaga Mheshimiwa
Makamu wa Rais alimwambia kuwa amefurahi sana kuwepo nchini Tanzania na
kwamba anaithamini nchi hii kama nyumbani kutokana na uwezo wake wa
kudumisha amani na pia kwa nafasi yake katika kuhakikisha wananchi wa
Msumbiji wanakuwa huru na wanaishi kwa amani kama ilivyo sasa.
Balozi
huyo alisema serikali ya Msumbiji inatumia fursa zake za kuhakikisha
inakuza kilimo ili kutoa nafasi ya kuwepo chakula cha kutosha nchini
humo na
pia
akafafanua kuwa hali ya kisiasa nchini mwake kwa sasa ni shwari na
hivyo wananchi wa ajukumu moja tu la kujitafutia maendeleo.
Balozi
Maricias alifafanua kuwa upo umuhimu wa kukuza nafasi za kubadilishana
wanafunzi kati ya Msumbiji na Tanzania kwani kama haitafanyika hivyo ni
rahisi wananchi wa nchi hizi kusahau historia ya namna nchi hizi mbili
zilivyoshirikiana katika kipindi cha kupigania uhuru.
Makamu
wa Rais alimueleza Balozi Maricias kuwa, Tanzania inashukuru sana kwa
mchango wake alioutoa kama Balozi na pia katika kazi alizofanya kabla ya
kuwa Balozi. Alimtakia kila la kheri katika kazi zake mpya huku
akimhakikishia kuwa Tanzania itabakia na mahusiano chanya na Msumbiji
katika kipindi chote.
Imetolewa: OFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)