Meneja
wa Sayansi na Uthibiti wa Nestle Tanzania Akikabizi zawadi kwa watoto
wa kituo cha kulelea watoto cha Chakuwama Orphanage Centre kama Sehemu
ya Kusheherekea siku ya Maziwa Duniani, Pamoja na watoto hao Pembeni ni
Mlezi wa Kituo pamoja na maofisa wakuu wa Biashara Kutoka Kampuni ya
Nestle Tanzania.
Mlezi wa kituo cha Kulea watoto yatima
cha Tanzania Mitindo House na Mwanamitindo Maarufu Bi Khadija Mwanamboka
akiojiwa na waandishi wa habari wakati akipokea zawadi kwa ajili ya
kituo cha watoto yatima cha TMH ambapo Kampuni ya Nestle kupitia bidhaa
ya NIDO imewawezesha vituo vitatu vya watuto yatima vya Dar es Salaam
kusherehekea Siku ya Maziwa Dunia kwa kuwapa Maziwa ya NIDO na Bidhaa ya
MILO zenye thamani zaidi ya TSZ 5 Milioni.
Bibi Mlezi wa Kituo cha CHAKUWAMA Bi.
Khadija alipokuwa akihojiwa na Muandishi wa Habari wa ITV Bw. Sam Mahele
Juu ya Changamoto wanazozipata katika harakati za uendeshaji wa Vituo
vya watoto yatima pamoja na Michango ya Taasisi mbalimbali kama Kampuni
ya Nestle NIDO ilivyofanya kuwawezesha watoto kuwa na afya bora na
kuhamasisha Unywaji wa Maziwa hali Ng’ombe yaliokatika mifumo mbali
mbali.
Bidhaa za NIDO, CereVita, MILO kutoka
Kampuni ya Kubwa ya Vyakula na Vinywaji Dunia ya Nestle zenye thamani ya
TZS 5,548,800 Zilizogawiwa kwa vituo vya Umra, Chakuwama na Tanzania
Mitindo house zenye watoto takribani 200 wanaolelewa na vituo hivyo
katika kuazimisha siku ya Maziwa Duniani ambayo hufanyika kila mwaka
Juni 1st.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya
Nestle Tanzania wakionyesha furaha yao baada ya Kujumuika na watoto wa
Vituo vya watoto yatima na kuchangia Vyakula kwa ajiri ya kuboresha afya
na maisha ya watoto hao kama sehemu ya kurudisha kwa jamii kwa kampuni
hiyo wakati wakisheherekea siku ya Maziwa Duniani Juni Mosi ya Kila
Mwaka.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)