(Moja ya makanisa yaliyochomwa Zanzibar hivi karibuni)
Ndugu zangu,
Afrika
mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa na hata kiongozi wa
kidini. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi binafsi na ya kundi dogo
badala ya yale ya kitaifa.
Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Hili ni jambo la hatari sana.
Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao. Kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.
Wahenga walisema ”kamba hukatikia pabovu”. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa.

Mahala
ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni
kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye
kamba inayotuunganisha Watanzania.
Mungu Ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)