Athumani
Hamisi
Tanzania
Standard Newspapers Ltd
P.O.Box
9033
Dar
es Salaam.
PRESS RELEASE
Mimi Athumani Hamisi
Awali
ya yote, napenda kuwasalimia wote, wakubwa na vijana wenzangu
Hii
itakuwa mara ya pili kuongea nanyi waandishi wenzangu, ndani ya miaka minne
tokea nipate ajali Septemba 12, 2008 eneo la Kibiti Mkoani Pwani nikiwa na
wenzangu Herry Makange ambaye kwa sasa ni marehemu na Anthony Siyame, tukiwa
njiani kwenda Kilwa mkoani Lindi kikazi.
Mara ya kwanza niliongea nanyi 2010 baada ya kurejea kutoka Afrika kusini
nilikopelekwa na Serikali kwa matibabu.
Shukrani
zangu za awali, zimwendee Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Kikwete aliyenitembelea katika Hospitali ya Muhimbili nilikolazwa na kuagiza
nilipelekwe nje kwa matibabu zaidi.
Katika
ajali ile, nilivunjika shingo na ku-damage spinal cord iliyopelekea kupooza
mwili wote kuanzia shingoni. Katika operesheni iliyofanywa na madaktari wa
hospitali ya Mil Park, Afrika Kusini walilazimika kuunganisha shingo kwa nyuma.
Shukrani
za pili ni kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kampuni ninayofanyia kazi ya magazeti ya serikali,
wachapishaji wa Daily News, Sunday news, Habari Leo Jumapili na Spoti leo,
familia yangu iliyokuwa katika wakati mgumu wakati huo hadi sasa watanzania wote
wuamini wa dini zote waliokuwa wakiombea Pamoja na marafiki zangu waliokuwa
wakihangaika huku na kule kwa namna moja ama nyingine .
Niko
mbele yenu leo kuwaomba mnifikishie ujumbe kwa jamii kwa maelezo yafuatayo:-
1.
Ofisi yangu ya
TSN ilinipangia nyumba ninayokaa Sinza Vatican, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar
es salaam Mei 2010-2011 na mkataba ulikukwa kati ya mwenye nyumba na TSN ambao
mimi sikuwahi kuuona hadi ninavyoongea na nyie leo.
2.
Mkataba uliisha
tena Mei 2011, mwenye nyumba alikwenda TSN kuomba kusaini mkataba mpya. Badala
yake aliandikiwa mkataba mpya wenye jina langu na kupewa aniletee mimi nisaini.
Nilipomuuliza mkataba wa kwanza uliingia na nani na ni nani alisaini. Alisema
ni TSN walisaini wakamwambia wana mgonjwa ambaye ni Staff wake atakuja kuishi
pale akitokea Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu. Mwenye nyumba akasema
walimwambia gharama za nyumba ni za TSN , sasa nashangaa leo wameandika jina
lako na mkataba ni kati yangu na wewe.
3.
Nikamwambia kaka,
mimi sikutarajia kufikia hapa kwani mwaka 1999 ilipangwa mimi nifikie katika
nyumba ya kampuni Upanga kuepusha gharama na ukaribu wa huduma za kitabibu,
mpaka masuala yangu yatakapothibitishwa na Daktrari kama hali yangu itaruhusu
mimi kuweza kufanyakazi ama vinginevyo. Rudi ofisini mkasaini kama mlivyofanya awali. Na umwambie
kwa hali ya Athumani hawezi kusaini mkataba na mimi kulingana na hali yake.
Isitoshe mi nilitiliana saini mkataba wa awali na TSN.
4.
Ukweli nilikataa
kusaini zaidi ya mara tatu, mpaka Meneja Mwajiri siyo huyo wa sasa alipoingilia
kati na kunithibitishia kuwa kampuni italipa nyumba mpaka uamuzi wa madaktari
utakapotoka, saini mimi nitakulinda. Niliporejea nyumbani nikawekwa wino katika
dole gumba wakaweka saini. Mpaka yalipojitokeza ya sasa.
5.
Ndugu waandishi
wa habari, hali yangu japo imeimarika zaidi kuliko awali, leo nimekuja na jambo
ambalo litahusisha jamii na nyie ndiye wahusika wakuu katika suala hili.
KIKUBWA ZAIDI LEO NI SHUKRANI NA OMBI
Ukweli
ulio wazi, nashukuru kwa Mungu na
kujivunia kuwa TSN . nimelelewa na TSN kwa miaka sita sasa. Imenilea nikiwa
mgonjwa kwa miaka mine, nikiwa bado niko ndani ya ajira jambo ambalo ni gumu
sana sehemu nyingine.
Imelipa
nyumba kwa miaka miwili na imesitisha kulipa kodi ya 2012-2013 kwa barua ya Februari 3,2012 na kutoa maelezo
kwenye barua kuwa imefikia hatua hiyo kutokana na kuwapa wafanyakazi wake
asilimia 15 ya mishahara yao kulipa nyumba. Nyumba walionipangia ni ya vyumba
viwili na kodi iliyolipwa kwenye mkataba wa mwaka jana ni Milioni 4.8
Nilipatwa
na mshutuko kidogo, nafsi ikanishauri niite menejiment nyumbani tushauriane
katika hili. Walikuja Machi 28, na wakanipa pole ya kampuni tokea nirudi 2010
Shs 50,000. Lakini mazungumzo hayakuisha kutokana na muda na kuahidi kurudi
wiki inayofuata kwa mazungumzo zaidi. Nimepewa notisi na mwenye nyumba April
23,2010.
Nadhani
kutokana na kubanwa na kazi, hawakupata nafasi ya kurudi tena kumalizia
mazungumzo. Kwa mtazamo wa kifikira ni wazi msimamo ulibaki palepale. Barua ya
kusitisha kulipa kodi haikuja kwangu tu bali pia mwenye nyumba alipata.
UFAFANUZI
Kabla
ya kuruhusiwa kurejea nyumbani Tanzania, Netcare Rehabilitation Hospital,
wanautaratibu mzuri sana. Kabla ya kuwa –discharged wanakuruhusu ukae nje ya
hospital kwa miezi mitatu, kama una mke au mume na kama huna utatafutiwa nurse
awe wa kike ama wa kiume mimi nilipata nurse. Baada ya hapo una hudhuria
mazoezi na vipimo kadhaa kwa miezi mitatu. Ukifaulu kumaliza miezi mitatu wewe
na mwangalizi wako hasa wewe mgonjwa bila kupata matatizo, hapo
wanaku-discharge.
Nilipiga
simu kwa Katibu Kiongozi Ikulu wakati huo, Philemon Luhanjo na kwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii anahitajika nurse kuja kukaa nami nje ya
hospital kwa miezi mitatu, je mtanisaidiaje? Kwa kweli jibu lao lilikuwa moja
tu hatutatuma nurse kutoka huku, tafuta huko huko, fedha za kumlipa, nyumba ya
kulala, chakula na usafiri, andika
budget itume haraka tutalipa na wasiliana na ubalozi waje kujua unakaa
wapi na fedha zitatumwa ubalozini
watakuwa wanakuletea.
Nilipata
nurse na miezi mitatu ilipokaribia kwisha nilifanya mawasiliano kujua kama
kutatumwa mtu wa kunifuata, wakanijibu njoo naye huyo huyo watanzania
waliofanikiwa kuangalia vyombo vya habari wengi walimuona kwani nilirudi Mei
28, 2010. Baada ya mwezi alimaliza mkataba name kutakiwa kutafuta nurse wa
kukaa naye kwa saa 24 . akapatikana na akafundishwa na M-South Africa jinsi ya
kukaa na mgonjwa wa Spinal Cord.
TSN,
wakamlipa nurse wa South Africa Rand 12,500 alizokuwa anadai na palepale
nikauliza vipi kuhusu malipo ya nurse
mpya ambaye ataachwa na mimi? Kwa sababu serikali imemaliza jukumu lake na
waliniambia kwa kuwa wewe bado ni mwajiriwa wa TSN, jukumu lote sasa utakuwa
chini yao na ndiyo mmepewa pia jukumu la kumlipa kama mlivyofanya leo. TSN
walinijibu palepalekuwa suala la kumlipa nurse ni lako na familia yako ila
nyumba tutalipa.
Vodacom walijitokeza kubeba gharama za tiketi nilipopata ajali kwenda Afrika Kusini na wasindikiaji wote, tiketi ya nurse niliyekuja naye. Pia wakalipa tiketi yangu na nurse Desemba 8,2010 kwenda na kurudi Afrika Kusini kwa ajili ya checkup.
Baada
ya TSN kulipa nurse yule msouth afrika, nikawapigia Vodacom Foundation kuwa
nurse amemaliza mkataba na ameshalipwa fedha naomba mumkatie tiketi. Hivyo ilikuwa Juni 25 na kesho yake Juni 26 2010
jioni wakaja watu wawili kutoka Vodacom Foundation na mmoja kutoka TSN
waliniambia wamekuja na vitu vitatu.
1.
Wakamshukuru nurse kwa kazi nzuri , lakini wakamwambia ,
sisi ni kutoka Vodacom. Vodacom
Foundation inakuomba uendelee kumhudumia Athumani . Na Vodacom watakulipa
mshahara lakina tunaomba upunguze kiwango.
2.
Yule nurse
akakubali akapunguza nusu ya mshahara aliokuwa akilipwa na serikali.
Wakamwambia sasa Vodacom Foundation inakata tiketi ya kwenda nyumbani Afrika
kusini kuaga. Akaomba siku 15, mkataba
wa mdomo ukakubaliwa na yule nurse na mshahara wa kwanza ukawa Julai
2010 kuendelea na kazi chini ya Vodacom. Julai 2010 wakamlipa. Kilichoendela
naomba nisiseme.
3.
Muda wa checkup
ulifika Desemba 2010, nikaitaarifu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Wakakubali wakaandika barua kwa kugawa majukumu. Afya wakasema watalipa
gharama za matibabu, Vodacom tiketi za
kwenda na kurudi na TSN waliagizwa kulipa allowance kwa mgonjwa na nurse.
Tukasafiri Desemba 8,2010 na tukarudi Februari 28,2011. Malipo yaliyofanywa na
TSN kidogo ni aibu naomba nisiseme.
4.
Hali hiyo
ilinionyesha kuwa Vodacom Foundation walikuwa wanatambua uwepo wa yule nurse.
Lakini hadi nurse anaondoka alilipwa mshahara mmoja tu na hata tiketi ya nurse
kurudi Afrika Kusini Vodacom hawakulipa.
5.
Nililipa tiketi
ya Business Class. Nikampa Rand 4,500 akakataa akachukua Rand 2,500 tu ,
akaniambia, Athumani nakuacha katika hali mbaya sana. Fuatilia haki zangu na
zako, ukifanikiwa utaniambia na Account ya benki , First bank nakuachia utaniwekea. Vodacom Foundation
hawajawahi kupokea simu yangu na Mkurugenzi wake hajawahi kupokea simu yangu
wala kuongea na mimi tokea nipate ajali.
6.
Suala lingine
waliniuliza nichague kitu kimoja, kujengewa nyumba au kusomeshewa watoto. Mimi
nilichagua kujengewa nyumba. Walichukua chaguo langu. Tukamaliza mazungumzo.
7.
Baada ya mwezi
waliniambia suala lako limekubaliwa ila tumepata Mkurugenzi mpya, lakini
usijali. Mpaka hapa ninavyoongea danadana ziliendelea mpaka ninavyoendelea
kwenye nyumba, sijawahi tena kupata jibu kutoka Vodacom. La mwisho nilijibiwa na mmoja wa watu wa
Vodacom Foundation aliniabmia wewe uliingia mkataba na kampuni ya One Plass na
si Vodacom Foundation.
SIKU YA LEO
Nimekuja
leo kuutangazia umma hali ilivyo. Ukweli kwa sasa Account ya CRDB ilikuwa maalumu kwa ajili ya kusomeshea watoto,
imekauka ya Postal bank ambayo ya
mshahara haina kitu. Pesa ya mshahara inayoingia benki ni 450,000
Nawalipa
nurse, msaidizi wake na mfanyakazi 370,000. Maisha ya ulemavu ni ghali
sikutarajia . nina wanangu watatu, wa kwanza anamaliza darasa la saba mwaka
huu, wa pili yuko la nne na wa mwisho yuko la pili.
Hawa
wanasoma primary za kulipia wote hawa nawalipia 200,000 kila mmoja kwa term
jumla 400,000 hizo shule zina term nne kwa mwaka. Gharama chakula, vifaa vya
wanafunzi, gharama zao ndogondogo na za kifamilia Pamoja na chakula kwa mwezi ,
inakwenda kati ya 750,000 mpaka 900,000 kwa mwezi.
Nimekuwa
ombaomba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei simu wala kujibu
sms . siyo siri ndugu wote wamekimbia
waliobaki ni marafiki wa kweli wameniingiza katika familia zao. Hali yangu ni
mbaya sana kiuchumi.
Sina
uwezo wa kulipa nyumba kwa gharama zozote zile. Mimi Athumani Hamisi, naomba
watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa nyumba na ushauri wa madaktari
walinishauri nisiishi mbali na mazingira ya hospitali kulingana na hali yangu.
Makampuni
, mashirika, wizara yoyote, shirika la nyumba la Taifa NHC, watu binafsi,
serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu nawaomba wanisaidie kwa
njia yoyote . kwa walio tayari naomba
misaada ipitie katika account No 01J2027048800 ya CRDB na Account No
010-00090488 ya Postal Bank
Kwa
wanaotumia mitandao ya simu, wanaweza kutumia M-pesa 0757 825 737, Tigopesa
0655 531 188 na Airtel Money 0784 531 118; M-Pesa 0767 298 888 ya Chris Mahundi
na Airtel Money 0686 710 977 ya Ephraim Mafuru
Athumani
Hamisi
0784
531 188 | 0655 531 188
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)