Deidre Lorenz na Rais wa IBF-USBA bala la Africa, Masharini ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mcheza sinema toka
Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za
Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na ndege
ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon
zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka.
Ujio wa Lorenz ambaye
amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big
Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake
umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake.
Akizungumza na
waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema
kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana
furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko
Tanzania. “Nimekuwa nautangaza sana ujio
wangu kwenye blog na tovuti yangu, wapenzi wangu pamoja na watu wengi wanangojea
kurudi kwangu nikawaambie niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye
ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz alisema kuwa
kwa miaka mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi nchi hiyo
jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.
“Sasa nimeona mwenyewe kwa macho yangu kuwa
kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na sio Kenya” alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye
jiji la New York City linalofahamika kama jiji la pesa (International Financial
Capital) la kimataifa. Lorenz ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages
iliyopo karibu na benki ya Standard Chattered mkabala na bustani ya Manispaa ya
Uhuru Park.
Mji wa Moshi na viunga
vyake vinarindima kwa ujio wa watalii wengi kutoka Marekani ambao wamekuja
kushiriki kwenye mbio hizi zilizojijengea umaarufu mkubwa kwa kuitangaza
Tanzania nchini Marekani. Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa na
Marie Frances mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamania wa Tanzania
nchini Misri.
Mbio hizi zimejijengea
umaarufu mkubwa na zimeshawahi kupata tuzo nyingi baadhi zikiwa zimetolewa na
Wonders of the World Magazine lenye wasomaji zaidi ya milioni 5 likiwa limezipa
nafasi ya 2 kama mbio zenye hadhi ya kukimbiwa duniani wakati jarida la Forbes la
Marekani lenye wasomaji wengi duniani
limeipa nafasi ya kwanza. Ndio maana Manispaa ya Moshi itampa barabara na
kuiita “Marie Frances Boulevard”mwaka 2009.
Mbio hizi hukimbiwa na
watalii wa Warekani wanaokuja Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea
mbuga za wanyama. Mt. Kilimanjaro Marathon zinajulikana kama 7 continental
races zikiwa zinakimbiwa katika mabara 7 ya dunia.
Ratiba ya Deidre
Lorenz inaonyesha kuwa kesho ijumaa atakitemnbelea kituo cha watoto yatima cha
Upendo kinachoendeshwa na watawa wa Precious Blood. Lorenz atakaa na watoto hao
na kuwasomea hadithi mbalimbali za watoto zilizoandikwa na Waltz Disney
mwandishi maarufu wa karne ya ishirini wa Marekani.
Siku ya jumamosi atatembelea
hospitali ya KCMC ambapo atakutana na manesi ili kuwapa shavu kwa kazi yao
nzuri wanayoifanyia jamii. Jioni ya jumamosi atahudhuria Pasta Party ambapo
atapata nafasi ya kukutana na wakimbiaji wengine na kuchagua namba ya kukimbia
kesho yake siku ya jumapili tarehe 24 juni.
Imetumwa na:
Grace Soka
Afisa Uhusiano
--
Mt. Kilimanjaro Marathon
Mt. Kilimanjaro Marathon
Technology House
35-38 Ghalla Road
Moshi - Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)