TASWIRA ZA MAJERUHI WA AJALI YA TEGETA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

TASWIRA ZA MAJERUHI WA AJALI YA TEGETA LEO


Mmoja wa majeruhi akiwa katika gari la kubebea wagonjwa tayari kupelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Majeruhi aliyeumia sehemu za kichwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mwananyamala.


Majeruhi katika ajali ya leo huko Tegeta akipatiwa huduma na wauguzi wa hospitali ya Mwananyamala.

Frank Mmari (34) mkazi wa Bunju 'A' akiwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kupata ajali iliyotokea Tegeta leo.

Lewina Selekwa akipatiwa huduma ya maji ndani ya hospitali ya Mwananyamala.

Lewina Selekwa akiwa na jamaa zake.

 Pichani juu ni majeruhi wa ajali iliyotokea leo Tegeta Kibaoni njia panda ya Wazo Hill jijini Dar es Salaam baada ya lori moja kuligonga basi la abiria kwa nyuma baada ya dereva wake kushindwa kuliongoza, hivyo kuliparamia basi. Kwa mujibu wa taarifa ya Mganga Mkuu Hospitali ya Mwananyamala, Dk Sophinias Ngonyani watu waliopata ajali katika tukio hilo ni 11, kati ya hao 2 wamefariki dunia na mmoja ametambuliwa na ndugu zake kwa jina la Halima Salim Msulwa (40) na mwingine ni mwanaume ambaye mpaka sasa hajajulikana jina lake. Wengine 3 wamevunjika mikono na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi, wakati waliosalia wamepata matibabu na kuruhusiwa. (PICHA ZOTE NA MAKONGORO OGING'/GPL)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages