Habari
zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa Kiongozi wa mgomo wa madaktari
Bw. Steven Ulimboka ameokotwa maeneo ya Mabwepande akiwa amepigwa
mapanga na hali yake ikiwa ni mbaya Fullshangwe imepata habari kuwa
kulikuwa na gari lililokuwa likipeleka katika hospitali ya TMJ Mikochezi
na lilipofika hapo walimhamishia kwenye Ambulance na kumuwahisha
hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu.
Fullshangwe
imewasiliana na Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Kamanda Kenyela hata
hivyo ilipokelewa na msaidizi wake ambaye amesema Kamanda Kenyela
amebanwa sana na kazi hivyo tumpigie baadae anaweza kuwa na muda mzuri
wa kulizungumzia suala hilo, Haijafahamika bado kama wahusika wa
shambulio hilo ni akina nani na tutaendelea kuwataarifu
kadiritutakavyopata taarifa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)