Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akitoa
ufafanuzi wa mradi wa mabasi yaendao mwendo kasi (DART) mei 2,2012 jijini
Dar es Salaam kwa waandishi wa habari hawapo pichani alipotembelea
na kuangalia maendeleo ya mradi huo ambao utagharimu shilingi
bilioni 288 za kitanzania ambazo zitajumlisha kwa pamoja na ujenzi wa
vituo vya mabasi.
Waziri wa Ujenzi Dr, John Magufuli (mwenye
koti jeusi) akikagua upanuzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta leo jijini
Dar es Salaam. (mwanamke ni ) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa DSM
Mwantumu Mahiza,na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango
(mwenyetai)
Mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS Mhandisi
Patrick Mfugale akitoa maelezo ya mradi wa DART Mei 2,2012
jijini Dar es Dar es salam kwa Waziri wa Uchukuzi Dkt. John Magufuli
(wapili kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa DSM Mwantumu
Mahiza, (kushoto). Mradi huo ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano
wa magari na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa jijijni.
Baadhi ya sehemu ya ujenzi wa daraja huko mbezi- mwenge- Tegeta. (Picha
na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
NA MAGRETH KINABO –
MAELEZO
WAZIRI wa Ujenzi , Dk.
John Magufuli amemtaka mkandarasi wa ujenzi
wa Barabara ya Mabasi yaendayo
kasi(DART) yenye urefu wa kilomita 21 na vituo vya mabasi 29 kutoka Kimara hadi
Kivukoni iliyoko Jijini Dares Salaam kufanya kazi usiku na mchana ili
kuhakikisha
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Magufuli leo wakati
alipotembelea miradi hiyo miwili ili kungalia shughuli za ujenzi ambapo alifurahishwa na kazi hizo huku
akiwataka wamalize kwa muda unaotakiwa.
“Mkandarasi unatakiwa kufanya kazi usiku na mchana ili kazi
ikamilike kabla ya wakati kampuni yenu ni kubwa kama kuna matatizo yoyote mtuambie
sisi serikali ili tuweze kuyashughulikia,” alisema Waziri Magufuli.
Waziri Magufuli pia ametoa muda wa siku saba kwa Shirika la
Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) na
Mamlaka ya (DAWASA) kuondoa
miundombinu yao haraka ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi wa DART.
Waziri wa Magufuli alitembelea ujenzi huo katika maeneo ya
Jangwani na Ubungo, ambapo alisema itagaharimu sh. bilioni 240 na ikijumwuishwa
na ujenzi mwingine wa vituo utagharimu
jumla ya bilioni 288 ambazo zimetolewa na Serikali na Benki ya Dunia.
Awali Meneja wa mradi , Frank Rohde kutoka
kampuni hiyo , alisema changamoto
inayoukumba mradi huo ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi huo kutoka bandarini
ambapo vimekaa kwa muda wa siku saba.
Akizungumzia kuhusu tatizo hilo Waziri Magufuli alisema
atazungumza na Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato(TRA) ili vifaa hivyo
vitolewe haraka.
Aidha Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi na Mshauri wa
upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Tegeta kutoka kampuni ya Konoike ya Japan kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa barabara hiyo
yenye urefu wa kilomita 12 inayogharimu sh. bilioni 88 kwa muda unaotakiwa na
kuacha kusingizio cha mvua kama wanavyodai kuwa umechelewa kwa asilimia saba.
“Mvua zilinyesha siku tatu haiwezi kuwa sababu kuna nchi mvua inayesha muda mrefu kuliko Tanzania
na ujenzi wa barabara unaendelea. Sijaridhika na hiyo sababu ninyi nchi za nje mnaweza kujenga hata mvua ikiwa inayesha. Ni
lazima wafidie muda … kuongeza kazi ya ujenzi hakutakuwa na ongezeko la muda
wala mtaji,” alisisitiza.
Wakati huohuo Waziri
Magufuli alitumia nafasi kuwataka wakazi wa Jiji hilo waliojenga katika maeneo
ya hifadhi za barabara hizo kuondoka wenyewe kwa kuwa sharia ni msumeno.
“ Tukikuta mradi unakwamishwa sisi tutabomoa.
Akizungumzia kuhusu mradi DART , Afisa Mtendaji wa DART Cosmas Takule alisema utatengeneza ajira
80,000 na kusaidia abiria 406,000. Mradi huo utakamilika katika kipindi cha
miezi 36.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam ,
Mwamtumu Mahiza alitka ajira hizo ziwe kwa vijana wa jiji hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)