Khamis Ngwali mfanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL akipokea
zawadi na cheti baada ya kuwa miongoni mwa wafanyakazi bora mwaka huu
katika Kampuni hiyo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapungia
mkono walishiriki wa maandamano mara baada ya sherehe za siku ya
wafanyakazi dunia hapo Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
Kulia ya Makamu ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mh. Mohd Aboud Mohd na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh.
Dadi Faki Dadi.
Mfanyakazi wa Wizara ya Afya kitengo cha Damu Salama Kisiwani Pemba Bibi
Sharifa Halifa akipokea cheti na fedha taslim akiwa miongoni mwa
wafanyakazi bora mwaka huu kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi.
Miongoni mwa Wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali Kisiwani Pemba
wakiandamana kusherehekea siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika
katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
---
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha Mazingira
mazuri ya Wafanyakazi hapa Nchini ambayo ndio yatakayotoa tija zaidi
katika sehemu mbali mbali za Kazi.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za siku ya
Wafanyakazi Duniani { Mei Mosi } zilizofanyika katika uwanja wa Gombani
Chake chake Pemba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alisema Seikali imesikia kilio cha Wafanyakazi na kwa kuwa sikivu
itajitahidi kuyafanyia kazi yale yanayowezekana katika kipindi hichi.
Alisema hatua ya kupandishwa kwa kima cha chini cha mashahara hivi
karibuni ni mwanzo wa hatua nzuri ya kuendelea kujenga mazingira hayo
bora ya Wafanyakazi.
Balozi Seif alifahamisha kwamba mfumko wa bei, kodi
kubwa na mishahara duni ni pigo kwa wafanyakazi ambao ndio ujumbe wa
mwaka huu utazingatiwa na malengo ya Serikali ya kukubaliana na kiwango
cha Mishahara cha shilingi 350,000/- yatafikiwa hatua kwa hatua
kulingana na hali ya Uchumi itakavyoruhusu.
“ Serikali itakuwa inajidanganya kwa kupuuza kwa kilio cha
wafanyakazi kwani nyinyi ndio wajenga Uchumi imara wa Nchi yetu.
Msipotunzwa vizuri na waajiri suala la kujenga uchumi imara litabakia
kuwa ndoto” Alifafanua Balozi Seif.
Akizungumzia suala la Elimu Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi aliwataka Wafanyakazi kuvitumia Vyuo Vikuu vya hapa
Nchini kukuza viwango vyao vya Elimu kwa lengo la kukabiliana na
Ushindani wa ajira.
Alisema hivi sasa kumekuwa na shindani mkubwa katika soko la ajira
ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapoTanzania ni Miongoni mwa
Mwanachama. “ Ushindani huu utakuwa mwepesi kwetu kama
tutajielimisha kwa bidii. Tusipofanya hivyo tutaachwa nyuma na hapo
hatutakuwa na mtu wa kumlaumu”. Alisisitiza Balozi Seif.
Alisema Suala la Elimu kwa mfanyakazi ye yote hapa Zanzibar ni la
lazima kwa lengo la kuliwezesha Taifa kufikia katika maendeleo ya
haraka.
Aliwasihi Waajiri wote kufuata taratibu za kumuhakikishia mfanyakazi
usalama wake mahala pke paa kazi.
Balozi Seif alisema iwapo waajiri watatumia vyema
taratibu hizo zinaweza kusaidia kupunguza gharama za matibabu, fidia,
uharibifu wa mali na kupote kwa muda wa uzalishaji.
Katika risala yao Wafanyakazi hao iliyosomwa na Nd. Omar Issa Omar
walisema pamoja na juhudi kubwa zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za
kuboresha maisha ya wafanyakazi lakini bado hali ni tete ya maisha ya
Wafanyakazi wa Zanzibar ambayo bado ni ya kubahatisha.
Waliiomba Serikali kuutumia utatu uliopo wa shirikisho la Wafanyakazi,
Waajiri pamoja na Serkali kuu kushirikiana katika kutatua matatizo
yanayowakabili Wafanyakazi.
“ Mshahara uliopo hivi sasa unakidhi pekee
mahitaji ya kununua ule mchele maarufu uliozoeleka kwa jina la
mapembe”.
Alisema Ndugu Omar Issa Omar. Wakizungumzia
kilio chao cha kutoelewa hatma ya Msingi wa Jengo lao pamoja na Matofali
walieleza nyoyo za Wafanyakazi zitashindwa kustahamili iwapo sulala la
jengo la Afisi ya wafanyakazi hao Kisiwani Pemba halitafikiwa.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/5/2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)