Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Ephraim
Mafuru akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumpata mshindi
wa gari aina ya Ford Figo, Pikipiki na Genereta katika droo ya mwezi ya
"Vumbua Dhahabu chini ya Kizibo" inayoendeshwa na kampuni ya bia ya
Serengeti, kwenye makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbaym kulia ni
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Diageo kanda ya Afrika Bi. Cristina
Diezhandino na kushoto ni aBakari Maggid Afisa msimamizi wa michezo ya
Kubahatisha.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Deagio kanda ya Afrika Bi.
Christina Diezhandino akibonyeza kitufe kwenye kompyua ili kuchezesha
bahati nasibu kwa ajili ya kupata mshindi wa gari aina ya Ford Figo leo.
Kampuni ya bia ya
Serengeti imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali hapa nchini kukabidhi
zawadi kwa washindi mbalimbali wa promosheni
kubwa na ya kipekee kabisa kutokea hapa nchini Tanzania ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ambayo ama kwa
hakika inashuhudia watanzania wengi wakinufaika na kupiga hatua mbele kimaisha.
Asubuhi ya leo droo ya nne
katika promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika
ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na
kupata kuhudhuriwa na waandishi
wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani
na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH
MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.
Kampuni ya bia ya Serengeti
kupitia vinywaji vyake aina ya
Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni
nchi nzima ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’ambapo kwa mara ya
kwanza wadau,washiriki na watanzania wote wameshuhudia mmoja wa washindi wa
droo ya nne akiibuka na gari mpya aina FORD FIGO huku mwenzake akichomoka na Jenereta
mpya.
Bi. Teddy Mapunda, Mkurugenzi wa mawasiliano
na mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti ( SBL) alikuwa na haya ya kusema“ najisikia furaha sana kuona kila
tunapochezesha droo yetu tunapata washindi ambao mpaka sasa tumeshawapata
washindi watatu wa jenereta,mshindi mmoja wa pikipiki na washindi wawili wa
Bajaj ambapo tayari tumewakabidhi zawadi zao,”alisema Mapunda
“ Bado tunaendelea kuwahamasisha wateja wetu na watanzania wote wenye
umri unaruhusu kshiriki katika promosheni hii waendelee kushiriki bila kukata
tamaa kwani bado kuna zawadi nyingi sana hadi zifikie milioni 780 kwa zawadi
pekeyake na milioni 380 pesa taslim
zinaendelea kushindaniwa.
Washindi
wetu katika droo ya nne ni Rogers Kavishe kutoka mkoa wa Kilimanjaro ambaye
amejishindia jenereta kupitia bia ya
Serengeti Lager, wa pili ni bw. Oktavian Changula kutoka mkoani Iringa ambaye amejinyakulia pikipiki mpya kupitia bia ya
Tusker lager wa tatu ni bw.Isack Juvenari kutoka mkoa wa
Morogoro ambaye amejishindia gari mpya
kabisa aina ya FORD FIGO
Kwa
upande wake meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Peter Chonjo aliwapongeza
washindi wote katika droo hiyo na kuwataka watanzania waendelee kunywa bia za
Serengeti ambazo zimeainishwa katika promosheni hiyo ili kuendelea kushinda na
hatimaye kupiga hatua katika maisha yao.
Kupitia
mawasiliano kwa simu ya mezani mshindi huyo wa gari mpya hakuweza kujieleza kwa
mara moja kutoka na hali halisi alioonekana nayo baada ya kupata taarifa ya
kushinda gari alipagawa na kupelekea mawasiliano hayo kuyumba kwa muda lakini
baadaye aliweza kutulia na kujieleza vizuri.Gari hilo litakabidhiwa kwa mshindi
huyo siku chache zijazo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)