Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh.John Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani leo asubuhi.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA),Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na Wanachana
wa Chama hicho pamoja na washabiki wake nje ya Mahakama Kuu kanda ya Dar
es Salaam leo mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili
kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
Wanachama wa Chadema pamoja na washabiki wa Mbunge wa Jimbo la
Ubungo wakishangilia ushindi wa kesi ya Mbunge wao,Mh. John Mnyika
Mnyika akipongezwa na Baadhi ya jamaa zake waliofika Mahakamani hapo.
Askari Polisi wakihakikisha usalama upo wa kutosha katika njia
walizokuwa wakipita wapenzi wa Chadema kusherehekea ushindi wa Mbunge
wao.Mh. Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani leo asubuhi.
Wafuasi na Wanachama Wa Chama Cha demokrasi na Maendeleo CHADEMA wakiwa kwenye maandamano katika barabara ya bibi titi mohamed kuelekea ubungo mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh John Mnyika Kuibuka Kidedea katika Kesi ya Ubunge wa Jimbo la Ubungo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge Jimbo hapo Bi Hawa Ng'umbi katika Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Mwaka 2010.Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog na Fununu Habari
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)