WAZIRI MAKALA AIKABIDHI BENDERA TWIGA STARS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI MAKALA AIKABIDHI BENDERA TWIGA STARS

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla  akimkabidhi Bendera ya Taifa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Stars wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo inayokwenda Addis Ababa Ethiopia kwenye mashindano ya soka ya Kombe la mabingwa wa Afrika kwa upande wa  wanawake.Kushoto kwa Waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa TFF Bw. Sanday Kayuni.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla  akimkabidhi Meneja wa Timu ya Wanawake Twiga Stars Furaha Francis kitita cha Dola za Kimarekani 3500 kama mchango wa Serikali kw timu hiyo inayokwenda Addis Ababa Ethiopia kwenye mashindano  ya soka ya Kombe la mabingwa wa Afrika kwa upande wa  wanawake.Katikati ni  Kaimu Mkurugenzi wa TFF Bw. Sanday Kayuni. ( Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)


Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Twiga Stars) inayotarajia kuondoka leo saa 11.05 jioni kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwenda Ethiopia imekabidhiwa Bendera ya Taifa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
 
Twiga Stars yenye msafara wa watu 24 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itacheza na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya mchujo kwa ajili ya Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu Equatorial Guinea.
 
Mechi hiyo itafanyika Mei 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa Addis Ababa wakati ile ya marudiano itachezwa Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars ikifanikiwa kuitoa Ethiopia itakuwa imepeta tiketi ya kwenda Equatorial Guinea.
 
Wachezaji walioondoka na kikosi hicho ni Amina Ally, Asha Rashid (nahodha), Ester Chabruma, Ettoe Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fadhila Hamad, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustafa, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Tamba, Mwapewa Mtumwa, Rukia Hamis, Semeni Abeid na Zena Khamis.
 
Kwa upande wa Benchi la Ufundi ni Charles Mkwasa (Kocha Mkuu), Nasra Mohamed (Kocha Msaidizi), Furaha Francis (Meneja wa Timu), Mwanahamisi Abdallah (Mtunza Vifaa) na Christina Luambano (Daktari wa Timu).
 
Twiga Stars ambayo msafara wake unaongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itarejea nyumbani Mei 28 mwaka huu saa 6 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
 
LIGI YA TAIFA KUANZA MEI 27
Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa sasa itaanza Mei 27 mwaka huu badala ya Mei 26 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali. Uamuzi wa kusogeza mbele kwa siku kuanza kwa ligi hiyo uliofanywa na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Mei 23 mwaka huu).
 
Timu 23 zitachuana katika kinyang’anyiro hicho kitakachofanyika katika vituo vya Kigoma (Uwanja wa Lake Tanganyika), Musoma (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume) na Mtwara (Uwanja wa Umoja) ambapo kinatarajia kumalizika Juni 13 mwaka huu.
 
Kituo cha Kigoma kina timu za Aston Villa ya Singida, Bandari (Kagera), CDA (Dodoma), JKT Kanembwa (Kigoma), Majimaji (Tabora), Mwadui (Shinyanga) na Pamba (Mwanza).
Ashanti United ya Ilala, Flamingo (Arusha), Forest (Kilimanjaro), Korogwe United (Tanga), Nangwa VTC (Manyara), Polisi (Mara), Red Coast (Kinondoni) na Tessema ya Temeke ziko kituo cha Musoma.
Kituo cha Mtwara kina timu za Kurugenzi ya Iringa, Lindi SC (Lindi), Mighty Elephant (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Mpanda Stars (Rukwa), Ndanda (Mtwara), Super Star (Pwani) na Tenende (Mbeya).
 
MALAWI YATUA KUIVAA TAIFA STARS
Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) inatarajiwa kuwasili nchini leo saa 10 jioni kwa ndege ya Air Malawi kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayofanyika Jumamosi (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
Mechi hiyo ni kwa ajili ya kuipima nguvu Taifa Stars kabla ya mechi yake mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini chini ya Kocha Kim Poulsen.
 
Malawi itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu ambapo Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
 
Malawi ambayo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko Mtaa wa Lindi na Sikukuu baada ya mechi hiyo itakwenda Zanzibar ambapo Mei 28 mwaka huu itacheza na Zanzibar Heroes.
 
Makocha wa timu zote mbili Taifa Stars na The Flames kesho (Mei 25 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages