KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MIRADI MKOANI RUKWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MIRADI MKOANI RUKWA

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Dkt. Henry Shekifu akisalimiana na wakandarasi wa Makampuni ya Aasleaff na Bam International wanaojenga barabara ya Laela-Sumbawanga kwa kiwango cha lami. Kamati hiyo ya Bunge ipo Mkoani Rukwa kwa zaira ya siku mbili ambapo itakagua miradi mbalimbali ikiwemo barabara za Tunduma-Ikana-Laela, Laela-Sumbawanga, Sumbawanga-Kasanga, Bandari ya Kasanga na Miundombinu ya Anga ambapo wataona eneo la Kisumba lililotengwa tangu mwaka 1984 kwa ajili ya kujengwa uwanja mkubwa wa ndege na pia wataona uwanja wa ndege wa Sumbawanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Dkt. Henry Shekifu wa tatu kushoto Meneja wa Tanroad Mkoa wa Rukwa Florence Kabaka na wajumbe wengine wa Kamati hiyo ya Bunge wakishika udongo uliochanganywa na Cement na kushindiliwa ikiwa ni mojawapo ya hatua kuelekea ujenzi wa kiwango cha lami katika barabara ya Laela Sumbawanga eneo la kyanda walipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Aasleff na Bam International wakiendelea na ujenzi wa barabara hiyo. Mpaka sasa kilomita zaidi ya 10 zimeshawekwa lami ya majaribio na kazi nzima katika barabara hii ya Laela - Sumbwawanga imeshafikia asilimia 37 hadi kukamilika kwake.
Umwagiliaji kuimarisha ujenzi ukiendelea.
Wafanyakazi wakiendelea kuchapa kazi, hapo wakiondoa kokoto kwa ajili ya kuweka surface nyingine.
Mhe. Shekifu na Kamati yake wakiangalia moja ya eneo lililoanza kupata nyufa katika baadhi ya maeneo yaliyoanza kuwekwa lami. Mwenyekiti huyo alimuasa Mkandarasi huyo mambo matatu moja ikiwa ni kupata taarifa rasmi yenye uhakika kutoka kwao kuwa ni lini mradi huo utakamilika ili wawatangazie wananchi wenye kiu kubwa na barabara hizo. Pili wahakikishe ubora wa barabara hizo unazingatiwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na tatizo la nyufa zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo yaliyowekwa lami. Na mwisho ni kuhakikisha suala la fidia kwa wananchi wanaostahiki linakamilika kuepusha usumbufu wowote ule. 
Picha ya pamoja kati ya Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye ni Katibu Tawala Masaidizi Miundombinu Francis Kilawe wa tatu kulia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Dkt. Henry D. Shekifu (Mb) Lushoto katikati. Wengine ni wajumbe wa Kamati hiyo kutoka kulia ni Haroub Shamis (Mb) Chonga Zanzibar, Eng. Ramo Makani (Mb) Tunduru, Juma Sururu Juma (Mb) Bububu Zanzibar, Rukia Kassim Ahmed (Mb) Viti Maalum Kusini Pemba na Herbert James Mntangi (Mb)Muheza

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages