Wanafunzi wahitimu wa kozi ya uhifadhi wa mazingira wapatiwa kompyuta mkoani Arusha - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wanafunzi wahitimu wa kozi ya uhifadhi wa mazingira wapatiwa kompyuta mkoani Arusha

Na Gladness Mushi wa Fullshangwe- Arusha

WANAFUNZI watatu waliohitimu mafunzo ya kompyuta katika chuo cha uhifadhi wa mazingira   cha University Times  Training  Insititute kilichoko Moivaro mkoani Arusha wamepatiwa kompyuta tatu zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili ikiwa    ni njia ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe baada ya kuhitimu mafunzo yao.

Wanafunzi hao wamekabidhiwa kompyuta hizo na  mkurugenzi wa chuo hicho Bw Solomon Njiamoja alipokuwa katika hafla  ya mahafali ya kwanza  ya wahitimu  wa  hoteli management na kompyuta   yaliyofanyika chuoni hapo.

Bw Njiamoja alisema kuwa chuo hicho kimeamua  kuwapa wanafunzi hao kompyuta hizo ili ziweze kuwasaidia katika kujiajiri wenyewe ambapo wataweza  kukabiliana na hali ngumu ya kimaisha kwa kuwa vijana wengi wanashindwa kutimiza malengo yao kwa ajli ya kukosa vitendea kazi.

Aidha aliongeza kuwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanahohitimu chuoni hapo wanapata mafanikio mazuri chuo hicho kinatarajia kutoa kompyuta 105 kwa mwaka ambapo kila mwanafunzi anayefanya vizuri katika somo hilo atapata kompyuta yake ya kumuwezesha  kujiajiri.

Mkurugenzi huyo akielezea malengo ya chuo hicho alisema kuwa kinatarajia kuanzisha redio pia kuanzisha mfuko maalum wa kuendeleza waalimu kwa kuwa walioko wana shahada ya kwanza hivyo haiwatoshelezi kutoa elimu .

Awali mgeni rasmi katika mahafali hayo diwani wa kata ya  sokoni one Maiko Kivuyo aliwataka wanafunzi hao kutumia kompyuta hizo vizuri   kwa kuzitunza na badala yake wasiziuze kwani wako baadhi ya vijana  wakipewa zawadi wanakimbilia kuuza ili wapate fedha.

Aliwataka vijana hao kutumia elimu hiyo waliyoipata vizuri kwa kuwa katika dunia ya sasa  hakuna kitu unachoweza kufanya bila kutumia  kompyuta.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages