MKUTANO WA WANACHAMA WA TAASISI YA WANAFUNZI WANAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA ULIOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUTANO WA WANACHAMA WA TAASISI YA WANAFUNZI WANAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA ULIOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI

Mwenyekiti Wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosomea shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) Emmanuel Misungwi akitoa ripoti na taarifa ya taasisi hiyo katika mkutano na wanachama uliofanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Gaudensia Mwakemwa akitoa ripoti ya ziara ya wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya Sosholojia walipotembelea hospitali ya Milembe iliyopo Mkoani Dodoma na Kutoa Msaada wenye Thamani ya Shilingi Laki Tano Na Nusu za Kitanzania.
Baadhi ya Wanafunzi Wanaosoma Shahada ya Kwanza Ya Sosholojia waliohudhuria Katika Mkutano huo ambapo Mwenyekiti na Baadhi ya Viongozi waliweza Kutoa Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Taasisi hiyo pamoja na kuzumgumzia Maswala Mengine yanayohusu Taasisi hiyo
Mwalimu Mlezi Mh Jeremia alipokua akitoa ufafanuzi juu ya maswala mbalimbali yanayohusu taasisi hii na kujibu baadhi ya maswali kutoka kwa wanafunzi wa taasisi hiyo katika mkutano uliofanyika mwishoni wa wiki.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages