Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Africa Century 4 Development (CC) Fred Simon
akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kuwakaribisha wakulima wa
kilimo cha kisasa kutoka makampuni 13 ya nchini Afrika Kusini ambao
wamekuja Tanzania kwa ajili ya matembezi ya kujifunza mbinu mbali mbali
za kilimo na kuangalia fulsa za kuikwamu Tanzania katika mpango wa
kilimo kwanza.
Bw. Simon alisema kuwa kilimo ni biashara inayolipa kwa kiasi kikubwa, hivyo ni vyema kila mmoja wao kufanya kazi kwa bidii.
Mkutano wa waandishi wa habari pamoja wakulima wa kilimo cha kisasa kutoka Afrika Kusini.
Wageni wakifuatilia mkutano huo.
Katibu
Mtendaji wa Tanzania Youth Agriculture Foundation (TYAF) Bw. Gasper
Mahekula akitoa maelezo machache ya taasisi yao mbele ya wakulima kutoka
nchini Afrika Kusini pamoja na waandishi wa habari ambapo
aliwakaribisha wageni hao kuwekeza katika kilimo.
Wa
kwanza kulia ni Mtaalam wa Mambo ya Utawala wa Kilimo wa Kampuni ya IIQ
ya Afrika Kusini Bw. Ockie Olivier ambaye ameongozana na wenzake
wakifuatilia mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. Braam Coetnee
(kushoto) wakiwa na mmoja ya wenyeji wao (katikati) pamoja na Kiongozi
anayehusika na mambo ya nje ya Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw.
John Luscombe jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Africa Century 4 Development (CC) Fred Simon
akifanya mazungumzo na waandishi wa habari mara baada ya mkutano jijini
Dar es Salaam.
Kiongozi
anayehusika na mambo ya nje ya Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw.
John Luscombe akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya
mkutano jijini Dar es Salaam. Picha/www.kajunason.blogspot. com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)