Miss Kurasini anaeshikilia taji ambaye pia ni Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.
SHINDANO
la Redds Miss Kurasini 2012, ambalo linataraji kufanyika Mei 25 mwaka
huu katika ukumbi wa Equator Grill, yamezidi kupata wadhamini
watakaofanikisha shindano hilo.
Akizungumza
jana Mkurugenzi wa ZUM Fashion & entertainment, Zuwena Mustapha
amesema mbali na Kampuni ya Bia Tanzania kudhamini shindano hilo kupitia
kinywaji chake cha Redds, pia makampuni kadhaa yamevutiwa na kuamua
kudhamini shindano hilo.
“Leo
napenda kuwaambia kuwa hadi sasa tunajumla ya wadhamini 14 ambao
wamejitokeza kudhamini shindano hilo, lakini bado milango ipo wazi kwa
yeyote anaependa kutuzamini na kusaidia warembo wetu wa kurasini kupata
zawadi nono na shindano kuwea zuri,”alisema Mustapha.
Mustapha
amesema wadhamini wakuu wa shindano hilo ni Nameems Wear wakisaidiwa na
Reds, Dodoma wine, Clouds FM, Lady Pepeta, Father Kidevu Blog, Jambo
Leo, Aucland Tours & Safaris, Candy Bureau de Change, Flexip, PJ
Amusement, Renzo Salon na Madishisha Video Production.
Aidha
Jumla ya warembo 16 wamejitokeza kuwania taji la Redds Miss kurasini
2012, ambalo taji linashikiliwa na Top Model wa Miss Tanzania 2011,
Mwajabu Juma.
Akiwataja
warembo waliopo kambini na kunolewa na Mwajabu Juma akisaidiwa na
Malkia wa vipaji wa Miss Tanzania 2011, Rose Hurbert ni Mariam Sadic
(19), Johari Juma (20),Linda Deus (20),Irene Sostheness 20),Neemadoree
Sylvery(29),Edna Magige (22), Lindanancy Joseph(20), Elizabeth Mkende
(19), Betty Peter (22), Jennifer Njabili (18), Lilian Joseph (20),
Farida Mrope (23),Christina Moses (20), Angle Gasper (19), Flaviana
Maeda(22) na Sia Kimambo (19).
Shindano
hilo la Urembo ya Miss Tanzania katika kituo cha Kurasini yanategemea
kupambwa na burudani kali kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao
watatangazwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)