Wabunge
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na
Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uwongozi wa tawi
la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas,
Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa
US, wakiiunga mkono bendera ya taifa.
Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Msigwa na Mhe.
Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, Usiku wa Jana Jumatano Mei
30,2011 waliagwa rasmi kwa kupelekwa kuangalia mechi ya Soka ya
kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo
Landover Maryland Nchini marekani. Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mchezo huo ilikuwa ni 67,656 wakiwemo Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa.
Wabunge
wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil
ndani ya uwanja wa Fedex Field, uliopo Landover Maryland Nchini
marekani.
Picha
ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil
Usiku wa kuamkia leo Alhamis ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover
Maryland Nchini marekani
Wabunge
hao wakishangilia na Bendera ya Taifa wakati wakishangilia Bao la
kwanza la Brazil lililofungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar.
Wachezaji
wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti US kwenye mechi hiyo ya
kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani
kwao.
US.
wakijishauri kuanza mtanange huo baada ya kuchapwa bao la nne bao la
kwanza lilifungwa na Neymar, na lapili na Thiago mnamo wa dakika ya 11,
kipindi cha kwanza. bao la US lilifungwa na Hercules Gomes dakika ya 44
kipindi cha kwanza hadi mapumziko Brazil 2 US 1.
Mshambuliaji
wa United States Landon Donovan, akipiga krosi huku akidhibitiwa na
Brazil defender Marcelo wa Brazi katika mpambano wa kirafiki.
Hivyo ndivyo ilivyo katika uwanja wa FedexFeild, uliopo Landover Maryland Nchini Marekani.Picha na swahilivilla.blog spot.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)