Wilaya Afisa Ardhi Wilaya ya Mvomero, Majaliwa
Jafari (mwemnye miwani kulia) akitoa maelezo juu ya ramani ya shamba
296 lililopo Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa
ya Mlali, Wilayani Mvomero mkoani Morogoro ambalo lina mgogoro baada ya
Mwekezaji wa Kizungu wa kudaiwa kuvamia mashamba ya wananchi na kufunga
njia inayounganisha kitongoji cha Kinyebnze na mwanga kijijini Kipera.
Kulia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha mwanga na katikati yao ni
Mwanakijiji Mroki Mroki.
Mafisa wa ardhi Wilaya ya mvomero wakiwa katika uhakiki wa mipaka hiyo kijijini hapo jana.
Wataalam wa upimaji wakiwa kazini
Akina mama na watoto wakifuatilia zoezio hilo.
Afisa
mtendaji wa kata ya Mlali, Said Said Mdume akizungumza na maafisa ardhi
na wananchi wa Kinyenze baada ya zoezi la upimaji kusitishwa kufuatia
wananchi kutaka zoezi hilo lifuate mchoro uliopo unaonesha mpaka wa
shamba hilo ni barabara ya waenda kwa miguu na lipo mbali na mto
Kinyenze na sio kama ilivyo pimwa na kuvuka mto.
Zoezi
hilo liliamuliwa kuendelea leo na kupima kipande kilicho na mgogoro
pekee. hata hivyo uchunguzi uliofanywa na father Kidevu Blog umebaini
kuwa Umiliki wa mzungu huyo katika shmba hilo si halali kufuatia Uongozi
wa kijiji kudai kuwa haukuwahi kutoa Muktasari kwaajili ya kupata hati
ambayo ilishamalizika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)