EDWARD LOWASA AMPONGEZA KIDUNDA AKIWA DUBAI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

EDWARD LOWASA AMPONGEZA KIDUNDA AKIWA DUBAI


KATIBU wa shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini BFT Makore Mashaga pamoja na makocha na viongozi wa BFT kwa pamoja wamempongeza bondia Selemani kidunda kwa kuteuliwa kushiriki mashindano ya Olimpiki yanayotarajia kufanyika hivi karibuni 
 
akizungumza katika afla hiyo ya kumpongeza na kumtia moyo kuendelea na mazoezi kwa ajili ya michunano ya olipiki inayokuja karibuni aidha Makamu mwenyeki wa BFT Michael Changalawe amemshukuli Waziri Mkuu Mstaafu Eduward Lowasa kwa kumpatia Kidunda Dola 100 baada ya kukutana Dubai wakati wanarudi Tanzania
 
kambi ya ngumi inaingia kambini kesho tarehe 10 katika uwanja wa ndani wa taifa kwa ajili ya mazoezi zaidi mbali na mashindano hayo timu hiyo imeomba wafadhili wajitokeze kwa ajili ya kuipa sapoti ambapo wanatarajia kwenda botswana kwa ajili ya kuweka kambi ya bondia Kidunda na wengine kupima Viwango vyao
 
alisema Makore timu inakabiliwa na uaba wa wafadhili hivyo kuwaomba watu binafsi mashirika pamoja na makampuni kujitokeza kusaidia mchezo wa masumbwi ili uweze kusonga mbele nchini kwa kutoa sapoti moja kwa moja kupitia mchezo wa ngumi kwa sasa kambi hiyo itakuwa na mabondia kumi kila uzito

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages