Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipera, Anthony Karoli (wapili kushoto) akiwa katika maoja ya shunguli za kijiji jana.
Na Mwandishi wetu, Mvomero.
Viongozi hao wa
Kijiji walikutana mapema wiki hii chini ya Mwenyekiti Anthon Karolin a
wakiwa katika mkutano wao wa kawaida wa Halmashauri hiyo ya kijiji
iiliibuka Agenda ya kumkataa Mtendaji huyo na kumtaka akibidhi ofisi
mara moja, kutokana na shutuma mbalimbali za kiutendaji dhidhi yake.
Habari
zilizoifikia blogu hii kutoka kwa wajumbe wa kikao hicho walidai kuwa
wamefikia uamuzi huo kutokana na kuona utendaji mbovu wa Mtendaji huyo.
“Kiukweli
huyu Mtedaji huyu hatufai na hatumtaki tena kijijini kwetu, maana
amekuwa kero na kwa uongozi wa kijiji na matokeo yake wananchi wanaulala
mikia uongozi wetu kuwa haufanyi kazi lakini kumbe anetukwamisha ni
mtedaji wa Kijiji,” alisema mmoja wa wajumbe.
Mjumbe
huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alidai kuwa miongoni mwa mambo
ambayo anashutumiwa mtendaji huyo ni pamoja na uaminifu, kutokuleta
maendeleo kijijini, na kuto tatua migogoro ya wananchi.
“Mtendaji
amekuwa si mwaminifu maana amekuwa akipokea fedha kwa wananchi za
michango lakini hazifikishi sehemu husika, na akiulizwa anakana kupokea
fedha hizo ilhali mtoaji anathibitisha kumpatia,” alisema mjumbe
Mwingine.
Pia
Mtendaji Makunga, anashutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa mwekezaji wa
Kizungu wa sghamba la kinyenze ili asishughulikie tatizo la mgogoro wa
ardhi kijijini hapo na badala yake kuwaambia wananchi kama wanataka
kushughulikiwa kwa mgogoro huo wachange Shilingi hamsini elfu.
Pia
inadaiwa kuwa miradi ya maendeleo iliyopo kijijini hapo ya Ujenzi wa
soko na kiwanda cha kusindika nyanya na matunda ambavyo vilianza ujenzi
wake na Afisa Mtendaji aliyefariki, hayati Ramadhan Maguo hajaviendeleza
kwa zaidi ya miaka 3 sasa na akiulizwa anadai kuwa Kipera sio kijiji
chake na hakuja hapo kuleta maendeleo.
Mbali
na shutuma hizo pia Mtendaji huyo anadaiwa kuruhusu kuwekwa kwa geti la
ukusanyaji ushuru kijijini hapo ambapo wananchi hata wakipita na mazao
yao ya shambani yakwenda kula hutakiwa kulipa ushuru na ushuru huo hauna
manufaa kwa kijiji kwakuwa unaenda halmashauri na Kijiji hakipati hata
senti.
Inadaiwa
kuwa Mtendaji huyo alipotakiwa kuachia ngazi na kurudi kwa mwajiri wake
na si kijijini hapo, alidai mbele ya baraza hilo la kijiji kuwa Kijiji
hakina mamlaka ya kumfukuza hapo isipokuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mvomero pekee.
Hata
hivyo Viongozi hao ambao walichachamaa na kumtaka aondoke aende kwa
huyo mwajiri wake na si Kipera maana mvomero ina vijiji vingi.
Kufuatia hatua hiyo wananchi wa Kipera wameupongeza uongozi wa kijiji chao na kuwataka wazidi kuwa wakali kwa viongozi ambao hawafanyi kazi zao na wamekuwa ni mzigo kwa kijiji.
Kufuatia hatua hiyo wananchi wa Kipera wameupongeza uongozi wa kijiji chao na kuwataka wazidi kuwa wakali kwa viongozi ambao hawafanyi kazi zao na wamekuwa ni mzigo kwa kijiji.
Source: www.mrokim.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)