Mojawapo ya darasa shule ya msingi selous (Darasa la sita)-Namtumbo
MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIDUGALO-Owini Mpangala (NAMTUMBO)
Na Vicent Mnyanyika, HakiElimu-Namtumbo
UHABA wa vyumba vya
madarasa ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili sekta ya elimu Wilaya
ya Namtumbo mkoani Ruvuma hali inayosababisha kushuka kwa kiwango cha
elimu wilayani humo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani hapa
baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule za msingi wilayani Namtumbo
wamesema wanatamani kuacha kazi au kuhama kutoka na changamoto nyingi
zinazowakabili kwa muda bila ya kupatiwa ufumbuzi. Wanasema kuwepo kwa
changamoto hizo za muda mrefu kuchangia kushusha kiwango cha elimu
katika shule nyingi za mjini.
Uchunguzi uliofanywa katika shule za msingi Rwinga, Selou, Mkapa na
Kidugalo zote kutoka Kata ya Rwinga umebaini shule hizo kukabiliwa na
uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa hali inayowalazimu walimu kujenga
vibanda vya nyasi ili kuwaepusha wanafunzi kukosa masomo kwa sababu ya
uhaba huo wa madarasa.
Hali hiyo pia imewalazimu walimu kutumia kutumia vyumba vichache
vilivyopo kwa kuwachanganya wanafunzi wa madarasa mawili katika chumba
kimoja hali inayotia shaka mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Mwandishi
ametembelea Shule ya Msingi Kidugalo na kushuhudia zaidi ya wanafunzi
200, wa kuanzia darasa la tatu mpaka la sita wanasoma katika vyumba
viwili vya madarasa huku wakiwa wamegeuziana migongo hali ambayo
inachangia kushusha taaluma katika shule hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ina shule za msingi 107 kati ya
hizo shule 105 zinamilikiwa na Serikali na shule mbili ni za watu
binafsi na mashirika ya dini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)