Aliyekuwa
Waziri wa Viwanda na Biashara wa zamani, Idd Simba akiongozwa na askari
Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam kujibu mashata 8 likiwemo la kula njama, kughushi,
kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na kulisababishia hasara
Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ya Sh. bilioni 2.3. Mshtakiwa huyo
alifikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengeni watatu.
Wakili Said Hamad El-Maamry (kushoto) akizungumza na Idd Simba Mahakamani hapo.
Mmoja
wa watuhumiwa katika kesi hiyo, Aliyekuwa Diwani wa Sinza, Salim
Mwaking'nda akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam jana mchana.(Picha
zote na Mpiga Picha wa Habari Mseto Blog).
Na Mwandishi Wetu
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya awamu ya Pili, Idd Simba ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la UDA jana amefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashata 8
likiwemo la kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu pamoja na kulisababishia hasara Shirika hilo ya zaidi ya
Sh. bilioni 2.3
Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengini watatu kutoka shirika hilo Idd Simba kwa makosa ya kughushi,kujipatia fedha kwa njia
ya udangayanyifu na kulisababishia hasara shirika la Usafiri Dar es
Salaam(UDA) shilingi bilioni 2.3. Mbali
na Idd Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA ,wengine ni
Mkurugenzi Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor
Milanzi wa shirika hilo ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea
Alex Mgongolwa na Said El Mamry ambapo upande wa Jamhuri unawakilishwa
na wakili wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa,Ben Lincol.
Mbele
ya Hakimu Mfawidhi Ilivin Mugeta ,wakili Lincoln alidai washtakiwa hao
wanakabiliwa na makosa nane.Alidai kosa la kwanza ni la kula njama
ambalo linamkabili Simba na Milanzi kuwa kati ya Septemba 2 mwaka 2009
jijini Dar es salaam walikula njama na watu wasiofahamika walitenda
kosa hilo kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na
Rushwa ya mwaka 2007.
Shitaka
la tatu ni la kuamisha fedha kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya
kupambana na Rushwa, kwamba Simba na Milanzi kwa tarehe hiyo Simba
akiwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Milanzi akiwa Meneja Mkuu
wa UDA,kwa pamoja walishirikiana kuamisha fedha kwa faida yao binafsi
sh 320,000,000,ikiwa ni malipo ya awali na ni sehemu ya ya malipo ya
hisa za UDA ambazo walizipokea wao binafsi kupitia nyadhifa zao .
washitakiwa wote wametimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo imeairishwa hadi Juni 28 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)