Kachero
kutoka Polisi Arusha, D/CPL Fortunatus (mwenye tisheti ya pundamilia
kushoto), akiimarisha ulinzi wakati Mtuhumiwa wa Kesi ya Wizi wa
Kuaminiwa, Bw. John Warburg (mwenye tisheti nyekundu), akiteremka
kutoka kwenye Bus la Ngorika katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini
Dar es Salaam Jana Mei 29.2012, wakitokea jijini Arusha ambako Mtuhumiwa
Warburg alikamatwa kufuatia kuruka dhamana aliyopatiwa katika Kituo cha
Polisi cha Urafiki takribani Miezi Mitatu iliyopita. John Warburg
alidhaminiwa katika Kituo cha Polisi Urafiki baada ya kukamatwa
akituhumiwa kwa kosa la kujipatia Gari aina ya Toyota Cresta GX 100
lenye namba za usajili T 796 AVQ na kuliuza kwa manufaa yake bila
idhini ya mwenye mali kesi yenye kumbukumbu namba URP/RB/2412/2012
-.URP/IR/1544/2012.
Mdhamini
wa Mtuhumiwa John Warburg bwana Max Kafipa (kulia), akiwa bega kwa bega
na mtuhumiwa wake kuhakikisha anafika Kituo cha Polisi Urafiki.Kushoto
ni D/CPL Fortunatus wa Polisi Arusha, aliyemu-escort mtuhumiwa hadi
hapa jijini.Picha na Daily Mitikasi Blog.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)