Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk.
Alberic Kacou akizungumza kwa niaba ya UNDP kuhusiana na kuzinduliwa kwa
Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 ambapo amesema huu sasa ni wakati
kwa nchi za Afrika haswa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kujenga
mazingira ya kuelekea mustakabali wenye uhakika wa chakula.
Mshauri
wa Uchumi UNDP Bw.Amarakoon Bandara akifanya 'presentation' ya Ripoti
hiyo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic
Kacou, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mkurugenzi wa UNDP
Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mratibu Mkazi wa Umoja
wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou (kulia) wakifuatilia maoni ya
Uchambuzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kutoka kwa Maprofesa wa
Vyuo vikuu nchini.
Dr.
John Mduma akifanya majumuisho ya nini kifanyike kukabiliana matatizo
ya uhaba wa chakula yanayolikabili bara la Afrika na Afrika Mashariki.
Profesa Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine akieleza uhifadhi wa Chakula kwa ajili ya matumizi ya baadae
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wadau wa Serikali wakichangia maoni yao kuhusiana na Ripoti hiyo.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) akisoma hotuba wakati
wa hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni
Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene (MB) akikata utepe kuzindua
rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
"Sasa
imezinduliwa rasmi" Mgeni rasmi Mh. Janet Mbene na Dk. Alberic Kacou
wakionyesha Ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari.
Baadhi
ya Wageni waalikwa wakipitia Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012
kuelekea kwenye Mustakabali wenye uhakika wa Chakula kwa nchi za Afrika
iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam
Bara
la Afrika ikiwemo Tanzania limeshakumbwa na matukio kadhaa ya
kukabiliwa na uhaba wa chakula, uliokwenda sambamba na matukio ya watu
wengi kupoteza maisha haswa Kusini mwa jangwa la Sahara na Ukanda wa
Sahel eneo la Afrika Magharibi.
Hali
hiyo imekuwa moja ya changamoto kubwa inazozikabili serikali za mataifa
hayo ambapo yanapambana ili kuitatua ili kila mwananchi barani Afrika
aweze kufurahia kukua kwa uchumi.
Akitoa
hotuba wakati akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 leo
jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) amesema
kwa muda mrefu sura ya eneo la nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa
la Sahara imekuwa ni ya njaa ya kukithiri, ambapo zaidi ya mtu mmoja
katika kila waafrika wane wana tatizo la upungufu wa lishe.
Amesema
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa pamoja na ukweli kwamba baadhi ya nchi
zinazokuwa kwa kasi kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ziko Afrika,
lakini bado hali ya maisha ya waafrika ni duni.
Awali
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania
Dk. Alberic Kacou alisema bara la Afrika limejaliwa kuwa na ardhi yenye
rutuba, maji ya kutosha na hali nzuri ya hewa kwa kukuzia mazao, lakini
swali la kujiuliza ni kwanini bado kuna uhaba wa chakula.
Hata
hivyo Dk. Kacou ametoa matumaini kuwa bara la Afrika bado lina uwezo wa
kujijengea mazingira ya kuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa kipindi
kijacho.
Ripoti
hii ya Kwanza ya Maendeleo ya Afrika inasema kwamba ongezeko endelevu
katika uzalishaji kwenye kilimo kunalinda haki ya chakula na uwezo wa
watu kupata chakula.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)