Spika
wa Bunge la Japan Takahiro Yokomichi ( kulia) akimkalibisha Spika wa
Bunge katika Bunge la Japan kwa lengo la kufanya mazungumzo kuimarisha
ushrikiano baina ya mabunge hayo mawili.
Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (katikati) akimsikiliza kwa
Makini mwenyeji wake Spika wa Bunge la Japan Mhe. Takahiro Yokomichi
wakati wa kikao cha pamoja kati ya ujumbe wa Bunge la Tanzania na Japan
walipo kutana Bungeni japan leo. Kulia kwa Spika ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Maliasili, ardhi na Mazingira Mhe. James Lembeli na
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Anne
Kilango. Ujumbe wa Bunge la Tanzania upo Japan kwa mwaliko maalum na
Bunge la Japan kwa lengo la kujadili na kuimarisha ushirikiano baina ya
Mabunge hayo mawili.
Ujumbe
wa Bunge la Tanzania ukiongozwa na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda
wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Bunge la Japan na ujumbe wa Bunge
la Japan ambao uliongozwa na Mwenyeji wake Spika wa Japan Mhe. Takahiro
Yokomichi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja kilichojadili
namna ya kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati ya Mabunge ya Nchi
hizi Mbili.
Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi ya picha
yenye wanyama (the Big Five animals) Spika wa Bunge la Ushauri la Japan
(President of House of Councilors) Mhe. Kenji Hirata wakati
alipomtembelea Ofisi kwake baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Ujumbe
wa Bunge la Japan na Tanzania.
Spika
wa Bunge akifanya mahojiano na Mwakilishi wa TBC aliyeko Radio Japan –
idhaa ya Kiswahili (NHK) Anna Kwambaza mara baada ya Spika na Ujumbe
wake kumaliza kikao na Mwenyeji wake Spika wa Japan, leo. Picha na Owen Mwandumbya
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)