Naibu Waziri, ajitolea kumsomesha aliyekosa ada Handeni - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Naibu Waziri, ajitolea kumsomesha aliyekosa ada Handeni

 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Ummy Mwalimu jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam. akiwa ofisini kwake wakati alipokutana na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi na kufanya mahojiano 
Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi akifanya mahojiano na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Ummy Mwalimu jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) akimadilishana kadi za mawasiliano na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com, Joachim Mushi mara baada ya mahojiano ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
 
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu jana amejitolea kumsaidia mtoto ambaye mzazi wake alishindwa kumpeleka shule baada ya kufaulu kwa kile kukosa ada ya shule.

Akizungumza na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi, ofisini kwake jijini Dar es Salaam amesema ameguswa na habari hiyo iliyotolewa na mtandao huu juzi, hivyo yupo tayari kumsaidia mtoto huyo nawengine watakao kuwa na matatizo kama hayo eneo hilo.

Hata hivyo, Naibu Waziri Mwalimu, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kutokea Mkoa wa Tanga amesema anaamini mama wa mtoto huyo alikuwa muoga kuwasiliana na viongozi wa wilaya hiyo ya Handeni kwani wangelimsaidia na mtoto huyo kujiunga na shule.

"Kwanza napenda kuwapongeza kwa kuibua changamoto kama hizi, kimsingi nimeguswa na habari hiyo ya mtoto kushindwa kujiunga na shule kwasababu mzazi wake hana uwezo...naomba mnipe mawasiliano ili tuangalie namna ya kumsaidia," alisema Naibu Waziri huyo.

Alisema ipo haja ya halmashauri kufuata ushauri wa Serikali kwa kile kutenga asilimia 5 ya mapato yao kuwawezesha wanawake kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake, kwani endapo akinamama watawezesha wanaweza kufanya mabadiliko hata katika changamoto kama hizo.

"Unajua ukimuwezesha mwanamke unakuwa umeiwezesha jamii...endapo kila wilaya ikikubali kutenga asilimia 10 ya mapato yake, kwa ajili ya mfuko wa  maendeleo ya wanawake na ule wa vijana kwa kugawa asilimia tano tano kila upande tutasaidia mambo mengi, zikiwemo changamoto za maisha katika familia," alisema Mwalimu.

Juzi mtandao wa Thehabari.com pamoja na mitandao mingine washirika wa Thehabari.com walichapisha habari ya mmoja wa wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na masomo mwaka huu kushindwa kuendelea na shule baada ya mzazi wake mmoja (mama) kushindwa kumgharamia.

Mtandao wa Thehabari.com unafanya mawasiliano na mzazi wa mtoto huyo na kuangalia namna ya kuwakutanisha na baadhi ya wasamaria waliojitolea kubeba mzigo wa masomo kwa kijana huyo. Mtandao huu utaendelea kuwajulisha taarifa zaidi za tukio hili hadi pale mtoto atakapo jiunga na shule.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages