Dkt.Engineer Shaban Kachua mwenye joho lenye rangi nyekundu na Bluu
(kulia) akiwa na waafrika wenzake baada ya kutunukiwa shahada zao,
wakati wa hafla ya kuwatunukia, ambapo Dkt. Engineer, alitunukiwa
Shahada yake ya Udaktari wa falsafa Nchini Canada.
Hapa Dr Kachua akiwa amekaa mstari wa mbele kabisa na wahitimu wenzake.
Mama
Mzazi wa Dr Kachua (mwenye blauzi nyeusi kulia), akiwa na Mama mkwe
wake, wote kwa pamoja walishiriki katika tukio la kihistoria la
kutunukiwa Shahada ya PHD kwa mtoto wao nchini Canada.
Mrs
Dr Shaban Kachua (Jemima) akiwa na furaha pamoja na watoto wao
walishiriki katika shughuli ya kutunukiwa Mume wake shahada ya udaktari
wa Falsafa (PHD).
Kwa
sasa Dr Shaban Kachua anaishi Nchini Canada pamoja na familia yake.
Sisi kama watanzania wenzake tunapenda kumpongeza sana kwa kuweza
kuipeperusha vema Bendera yetu, tunapenda kumshauri pia, elimu yake hiyo
aweze kuitumia pia kulisaidia Taifa lake la Tanzania hasa katika nyanja
hiyo ya Sayansi, kwa kutambua zaidi tuna upungufu mkubwa wa wanasayansi
katika Taifa letu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)