Makamu
akiwasili kwenye uwanja wa chipukizi mkoani tabora kufunga awamu ya kwanza ya
maandalizi ya sensa ya watu na makazi
iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia
wananchi wa Mkoani Tabora wakati akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa
ya watu na makazi iliyofanyika leo, Katika Uwanja wa Chipukizi
mkoani Tabora.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunga
kitambaa juu ya ramani ya Tanzania, kuashiria kufunga Awamu ya kwanza ya
maandalizi ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo, Mkoani
Tabora. Zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na Makazi inatarajia kuanza Tarehe 26 Mwezi Agosti, mwaka huu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea
zawadi ya Picha ya Ramani ya Tanzania, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ramani
Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Vincent Mugaya, baada ya kufunga Awamu ya kwanza ya
maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa
Ramani ya makazi itakayotumika na Makarani katika zoezi la kuhesabu Sensa ya watu
na makazi, na kusikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sensa, Hajat Amina Said
Mrisho, wakati Makamu alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa
ya watu na makazi iliyofanyika leo.
Sehemu ya wakazi na sungusungu wa mkoani Tabora wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal.
Kikundi cha kwaya cha JKT, kikitoa burudani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)