BASI LA KAMPUNI YA MURO INVESTMENT LATEKETEA KWA MOTO MKOANI MOROGORO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BASI LA KAMPUNI YA MURO INVESTMENT LATEKETEA KWA MOTO MKOANI MOROGORO

Basi la  Kampuni ya  Muro Investment, T820BEY lillilokuwa klikitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku Mei 8,2012, haikusababisha madhara kwa abiria ispokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo.
Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.
 Hapa Matairi yakiteketea kwa moto baada ya basi hilo kulipuka na kuungua lote.
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.
Wakazi wa Maseyu na wasafiri wakiangalia basi hilo likiteketea kwa moto.Picha/Habari Kwa Hisani Ya http://www.mrokim.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages