Mkrugenzi
wa kampuni ya LG kwa upande wa Tanzania akiongea na wageni waalikwa
waliofika katika uzinduzi wa Kinyoyozi kipya aina ya MULTI-V 3,
vinavyosambazwa na kampuni ya Alshaaf ambao ndiyo wakala pekee rasmi wa
kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG hapa Tanzania. Uzinduzi
huo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Fundi
mkuu wa Kampuni ya Alshaaf ambao ndiyo wasambazaji wa kiyoyozi kipya
aina ya MULTI-V 3 Bw. Emmanuel Myollah akiwahakikishia ubora wa viyoyozi
hivyo wageni waliofika katika uzinduzi huo.
Msajili Msaidizi wa bodi ya wahandisi nchini engineer Fares Washa akitoa machache katika uzinduzi guo.
Msajili
wa bodi ya wahandisi nchini engineer Steven Mlote akitoa machache
katika uzinduzi huo. Ambapo aliwashukuru kampuni ya LG kwa kuleta
teknolojia mpya ya viyoyozi aina ya MULTI-V 3 na vyenye ubora wa
uhakika.
Warembo wakifungua kwa taratibu pazia zilizokuwa zimefunika kiyoyozi huo ili kuashiria uzinduzi.
Wakiendelea kuvuta kwa taratibu...
Warembo wakiwa wameshafanya kazi yao ya usinduzi.
Kiyoyozi aina ya MULTI-V 3.
Wakurugenzi wa kampunya LG na Wahandishi wa bodi ya Wahandisi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi.
Wageni wakibadilisha mawazo katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya LG wakifuatilia uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
Umati wa watu uliokuwa umefurika kufuatilia uzinduzi huo.
Alshaaf
ni wakala pekee rasmi wa kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG
hapa Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
---
Tanzania imechaguliwa kuwa moja kati ya nchi pekee chache barani Afrika
ambapo LG imeamua kuzindua viyoyozi aina ya MULTI-V 3, ambazo ni toleo
la tatu (tabaka la tatu) la aina ya viyoyozi aina ya VRF Air
Conditioning bora kwa matumizi ya majengo ya biashara na makazi ya saizi
ya kati.
Viyoyozi
vya Multi- V 3 vinafaida tatu kwa kuu kwa watumiaji ikiwemo ufanisiwa
hali ya juu, uwezo mkubwa zaidi na faida ya kuwa na bomba refu.
Kampuni
la LG linalenga kubuni na kukuza bidhaa zinazotumia nishati kwa
ufanisi, natamka kwa kujivuna kwamba bidhaa hii itakidhi matakwa bora ya
wateja pamoja usalama wa bidhaa kutokana na teknolojia ya udhibiti
umeme na zaidi kutokana na faida za utunzaji wa mazingira kwa viwango
vya kisasa.
Alshaaf
ndio wakala pekee rasmi wa kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya
LG hapa Tanzania, naamini kwamba nchi yetu itaongoza katika kulinda
viwango vya kimataifa vya utunzaji wa tabaka la hewa na utunzaji
mazingira. Katika kipindi hiki cha mtikisiko wa upatikanaji nishati
duniani, bidhaa za LG zimeundwa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa
zinazolinda matumizi ya ziada ya nishati.
Tunawapongeza
washirika, LG na Alshaaf kwa jitihada zao endelevu za kutoa huduma za
ueledi za viyoyozi Tanzania kwa miaka 25 sasa na kujenga njia
inayoruhusu LG kuwa imara Tanzania kama wakala wao rasmi.





Ni wapi anapatikana?
ReplyDelete