KAMATI YA MISS TANZANIA YATANGAZA SHINDANO DOGO LA KUMSAKA MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA DUNIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMATI YA MISS TANZANIA YATANGAZA SHINDANO DOGO LA KUMSAKA MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA DUNIA

LINO INTERNATIONAL AGENCY LIMITED
P.O. BOX. 53069 DAR ES SALAAM, TELEFAX :+255 22 2120201,
SAMORA AVENUE AND MKWEPU, MOBILE: +255 753 764156,   DAR ES SALAAM.
www.misstanzania.net
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABAR
29 MEI 2012

WAREMBO wanaotaka kushindana katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 

.Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga amesema  kuwa wanatarajia kufanya mchujo wa washiriki Juni 5 kwa ajili ya kubakiza warembo 10 kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye ukumbi wa Dongsheng Fitness Center Stadium,  mjini Ordos, Inner Mongolia, China.

Lundenga alisema kuwa  zoezi hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la Serikali na  wakati huo, jumla ya warembo 12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za kushiriki. Alisema kuwa muda wa kufanya mashindano hayo umekaribia na wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi karibuni.

Alisema kuwa amefurahishwa na kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo wanahitaji warembo wengi zaidi ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya kumsaka mrembo atakayewania taji la Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian Sarcos.

“Tunakaribia kufanya mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu kuwakumbusha warembo wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya Juni 4 ili kuweza kuingia katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga.

Alisema kuwa mpaka sasa jumla ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa ajili ya mashindano hayo. Nchi 32 pamoja na Tanzania bado hazija chagua wawakilishi wao katika mashindano hayo.

 Fomu za kuomba kushiriki zinapatikana katika ofisi za Miss Tanzania za jijini na mawakala wote wa mashindano hayo katika mikoa ya Tanzania Bara.

HIDAN .O. RICCO.
PRO.
LINO INTERNATIONAL AGENCY LIMITED
0715 019288

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages