Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na wa Waziri wa Maendeleo wa nchini Finland, Heidi
Hautala (wa pili kushoto kwa Makamu) aliyeongozana na ujumbe wake
wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo asubuhi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na wajumbe walioongozana na Waziri wa Maendeleo wa
Finland, Heidi Hautala (wa pili kutoka kwa Makamu) baada ya kumaliza
mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam leo
asubuhi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Waziri wa Maendeleo wa
Finland na Ujumbe wake mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo asubuhi.
*********************************
*********************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA FINLAND
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
amekutana na Waziri wa Maendeleo wa Finland Mheshimiwa Deidi Hautala
ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano na maendeleo
wa nchi hizi mbili.
Katika
mazungumzo hayo Dk. Bilal alimweleza Waziri huyo hatua zinazochukuliwa
na serikali ya Awamu ya Nne katika kufikia dira ya Taifa ya maendeleo
2025 ikiwa ni pamoja na kutekeleza kauli mbiu ya kilimo kwanza na
kuhakikisha kila mtoto anapata elimu.
Alisema
katika kutekeleza kilimo kwanza, serikali inafanya jitihada ya
kuhakikisha maafisa ugani wa kutosha wanapatikana ili kusaidia wakulima
vijijini kujua mbinu bora za kilimo cha kisasa na namna
zitakavyowawezesha kuzalisha kwa tija.
“Hata
hivyo, tunajaribu kuongea na taasisi za fedha waweze kuwasaidia
wakulima kwa kuwapatia mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao,”
alisema na kuongeza
“Tuna
tatizo la soko kwani vijiji vingi havijaunganishwa na barabara, bado
tunawapa msaada wa kutosha kuhakikisha mazao yao yanafika sokoni.
Tunaamini kupitia kilimo kwanza tutawawezesha wakulima wetu kutoka
kwenye kilimo cha mashamba madogo na kwenda kwenye mashamba makubwa ya
biashara.”
Alipotakiwa
kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya hivi karibuni ya Baraza la Mawaziri
Dk. Bilal alisema hali hiyo inatokana na serikali kutoa madaraka kwa
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali na kuruhusu Bunge kuwa
huru zaidi.
Makamu
wa Rais alimhakikishia Waziri huyo kuwa, wale wote watakaobainika na
ubadhirifu wa mali za umma watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na
kusema kwamba serikali inatambua kuwa Mahakama ni chombo muhimu na
kamwe hakuna mwenye mamlaka ya kuingilia katika kutimiza majukumu yake.
Akiwa
nchini, Waziri Hautala ambaye anafuatana na ujumbe wa watu 12
anatarajia kuhudhuria mkutano wa Benki ya Maendeleo Afrika
utakaofanyika mjini Arusha.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es slaam
Mei 29, 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)