Waziri
wa Nishati na Madini Mh. Willian Ngeleja akitoa maelezo kuhusu
maonesho ya kimataifa ya vito ya Arusha kwa mwaka 2012 ambapo amesema
maonesho hayo yatawakutanisha wafanyabiashara wa madini ya vito kutoka
nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, pamoja na wataalam wa
kimataifa wa madini ya vito, wawakilishi wa serikali na wadau wengine
wa tasnia ya vito. Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini Ally Samaje.
Kaimu
Kamishna wa Madini Ally Samaje akijibu maswali ya waandishi wa habari
ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwa kuwa kupitia
maonesho hayo ya kikanda, nchi husika zitaweza kuonesha rasilimali
zilizopo na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuendeleza shughuli za
uongezaji thamani katika madini ili kuleta manufaa zaidi kwa nchi husika
kwa namna endelevu zaidi. Katikati ni Waziri wa Nishati na Madini Mh.
Willian Ngeleja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Adam Malima.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)