Mkurugenzi
Mtendaji wa Clouds Media Group ,Bw.Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni
wake,Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Tunu
Pinda mara alipowasili mapema leo asubuhi kwenye ofisi hizo.
Mke
wa waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda (pili kulia) akiwa amepozi katika picha
ya pamoja na Watangazaji wa kipindi cha Power breakfast kutoka Clouds FM
mapema leo asubuhi,Mama Pinda alifika kwenye ofisi za redio hizo kwa
ajili ya kuwahamasisha jamii mbalimbali kuisaidia timu ya Taifa Queens
kwenye michuano yake inayotarajiwa kuanza hivi karibuni hapa jijini
dar.Kutoka kulia ni Gerald Hando,Barbla Hassan pamoja na Paul James.
Mama
Tunu Pinda akiwa ni mmoja wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali
wameamua kushiriki kuihamasisha jamii na wadau mbalimbali kuisaidia timu
ya mpira ya wanawake ya Netboli (Taifa Queens ) kuhakikisha
inafanikisha malengo yake na pia kuhakikisha maandalizi yote yanakwenda
sawa.Pichani ni Mama Tunu Pinda akizungumza leo kwenye kipindi cha Power
breakfast kupitia redio ya Clouds FM jijini Dar kuhusiana na mchakato
mzima wa kuisadia Taifa Queens,kulia ni Paul James a.k.a PJ.
Taifa Queens kwa sasa iko kambini kwa ajili ya maandalizi ya mashidano ya Netiboli
ya Kombe la Afrika,ambapo Tanzania kupitia CHANETA imepewa heshima ya
kuandaa Mashindano ya Netiboli ya Kombe la Afrika ambayo yanatarajiwa
kuanza Mei 8-12, mwaka huu. Mama Tunu Pinda aliweka bayana kuwa gharama
za kuendesha mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 127.
Hivyo
Mama Pinda amewaomba wadau mbalimbali kuisaidia timu hiyo kwa hali na
mali ili iweze kufanya vyema kwenye michuano yake,aidha amewataka Wadau
watakaokuwa na nia kuichangia timu hiyo basi watume michango yao kupitia
namba ya simu 0779 000 808 (huduma ya Easy pesa),ambapo mtu ama kampuni anaweza kutuma kwenye namba hiyo kwa mitandano yote.Picha zaidi Bofya hapa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)