Mtayarishaji
wa muziki nchini Tanzania,Man Water (Man Maji),anaendelea na program
yake aliyoianzisha ya kutoa zawadi kwa wasanii ambao watakuwa wamerekodi
katika studio yake ya COMBINATION SOUNDS,na nyimbo za wasanii hao
kuweza kufanya vizuri katika vituo vya redio hapa nchini na nje ya nchi pia.Program
hiyo ambayo yeye mwenyewe ameita ni kutoa shukrani kwa wasanii ambao
kwa namna moja wanakuwa wanaitangaza studio yake vyema na kumfanya yeye
mwenyewe kuweza kujulikana na kupata kazi nyingi zaidi,aliinza kwa
msanii 20 percent,ambapo alikuwa ndio msanii wa kwanza kuweza kupewa
zawadi na Man water,Kwa kumnunuliwa baadhi ya vyombo vya muziki.
Mwaka
huu pia,Man Water tayari ameshatangaza nia yake hiyo ya kutoa zawadi kwa
wasanii wawili waliorekodi nyimbo zao katika studio yake ya COMBINATION
SOUNDS.Amemtaja msanii wa kwanza kuwa ni ALLY KIBA,msanii ambaye nyimbo
yake ya DUSHELELE iliweza kufanya vizuri na kukubalika sana.Dushelele
ni nyimbo iliyoweza kufanya vizuri na kushika chati mbalimbali katika
radio stations na Tv stations za hapa nchini Tanzania na
hata nnje ya nchi.Man Water amemuelezea msanii Ally Kiba kuwa ni msanii
mzuri mwenye kipaji na anaamini kwamba ni mmoja kati ya wasanii waliopo
nchini Tanzania ambao wanaweza kuufanya muziki huu kuwa bora zaidi na
kuutangaza nje ya mipaka ya Tanzania kwa urahisi zaidi.Pia amesema
anaamini ataendelea kufanya kazi na msanii huyu ili kuweza kutengeneza
nyimbo zenye ubora zaidi na kuendelea kuwaelimisha na kuwaburudisha
wapenzi wa muziki huu wa
kizazi kipya.
MBATIZAJI,ni msanii wa pili aliyetajwa na Man Water kuweza kupewa zawadi,baada ya nyimbo yake ya HESHIMA KAZI kuweza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na television vya hapa
nchini.Man Water,amemuelezea Mbatizaji kuwa ni mmoja kati ya wasanii
wenye tungo zenye maadili na kufundisha jamii.Amesema mara ya kwanza
alikutana na Mbatizaji (kipindi hicho akijulikana kwa jina la MASTA’
BROS) mkoani Morogoro mwaka 2003 na kuweza kusikia nyimbo zake kama
“BARUA KWA MAMA” na “NINI MAANA YA MAISHA” na kuona uwezo
mkubwa alionao katika utunzi wa nyimbo zake,ndipo mwaka 2005,wakati Man
Water akiwa anafanya kazi katika moja ya studio zilizopo mkoani
Morogoro,akamrekodia nyimbo iliyojulikana kwa jina la “KIPI
HASA?”,nyimbo aliyoipiga ama itengeneza katika midundo ya kapuka(staili
toka Uganda).Mwaka jana Mbatizaji
aliingia katika studio za COMBINATION SOUNDS na kutaka kurekodi wimbo
wa HESHIMA KAZI.Man Water alifurahishwa sana na ujumbe uliopo ndani ya
nyimbo hiyo na kummwagia sifa nyingi msanii huyu,ndipo wakati akiwa
anamuelekeza MBATIZAJI baadhi ya sehemu,wakajikuta wakiamua kuuimba
wimbo huo pamoja ili kuupa radha zaidi na ubora zaidi.
“Unajua
ninaufahamu uwezo wa Mbatizaji mda tu,so kwa nyimbo bora kama ile
ilinipa hata mimi mzuka wa kuweza kuimba na kurekodi,na naamini
hatutoishia katika heshima kazi tu,tuna plan yakuja kufanya kitu tofauti
zaidi,kwanza kwa taarifa yako ujue mshkaji nae ni mtayarishaji wa
muziki pia,so huwa najisikia kama nafanya kazi na mtu anayefahamu
mambo”.Alisema Man Water.
Man
Water hakutaka kuweka wazi ni zawadi gani atakazotoa mwaka huu,ila
amesema muda utakapofika kutokana na ratiba zake,atawaita wasanii hawa
na waandishi wa habari,na kuwakabidhi zawadi hizo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)