Balozi
mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Sano Lambert (katikati)
akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari
yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Katika Ujumbe wake ameitaka Jamii
ya Wanarwanda na Dunia kwa ujumla kuchukulia tukio hilo kama
changamoto ya kudumisha amani na upendo duniani na kutaka Mataifa
duniani kote kuishi bila itikadi za Kikabila. Kulia ni Afisa Habari wa
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo na kushoto ni
First Secretary wa Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania Bw. Ernest
Bugingo.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo
akizungumzia maadhimisho hayo yatakayofanyika tarehe 7 mwezi huu ambapo
amesema vyombo vya habari ni sekta muhimu ambayo inapaswa kuhudhuria
pamoja na jamii nzima kutazama filamu fupi ya dakika 7 inayoonyesha
kilichotokea wakati wa mauaji ya kimbari. Kulia ni Afisa kutoka Kitengo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama na Kushoto
ni Balozi Mdogo wa Rwanda, Mh. Sano Lambert.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)