Mwenyekiti
wa chadema,Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi kuu ya Upinzani Bungeni
Mh Freeman Mbowe akiongea na wananchi waliouhudhuria mkutano huo katika ofisi ya chama
hicho mara baada ya mahakama kutengua ubunge wa Godbless Lema jijini
Arusha leo.
Mwenyekiti
wa chadema Freman Mbowe katikati akitoa hotuba yake kwa wananchi
kushoto ni mbunge mteule wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nasari
na kulia ni Godbless Lema aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini
mara baada ya hukumu kutolewa.Picha na Habari na Gladnedd Mushi-Arusha
---
KATIKA Hali isiyokuwa ya kawaida MBUNGE wa jimbo la Arusha mjini Bw Goodbless Lema ametenguliwa na mahakama kuu kanda ya Arusha katika matokeo yake ya ubunge na kisha mahakama hiyo kutangaza hadharani kuwa siyo mbunge
Akisomewa hukumu hiyo mapema leo na jaji mfawidhi kutoka katika kanda ya sumbawanga Jaji Gabriel Rwakabirira alisema kuwa ameridhika na ushahidi wa pande zote mbili na ndio maana ametoa hukumu
Jaji Gabriel alisema kuwa alipokea dondoo 10 kutoka kwa wafuasi wa CCM ambapo alifanikiwa kukubali dondoo 8 na kisha kukataa dondoo nyingine mbili kwa mujibu wa sheria na taratibu za mahakama.
Alisema kuwa Mbunge Lema alitenda makosa hayo kati ya mikutano 60 ambayo aliifanya katika enzi za kampeni za mwaka 2010 ambapo alimchafua Mgombea Mwenza ambaye ni Dkt Batilda Burian kinyume cha
sheria
Jaji huyo alifafanua kuwa mbunge huyo alikutwa na makosa nane hali ambayo inamfanya mpaka sasa ang'atuke kwenye ubunge kwa mujibu wa sheria na taratibu za mahakama.
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa anamuagiza msajili wa mahakama wa kanda ya Arusha kuhakikisha kuwa anapeleka taarifa kwa tume ya uchaguzi juu ya kuenguliwa kwa Mbunge huyo lakini bado yuko huru kukata rufaa hata kwa ngazi za juu sana.
Awali Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Arusha Mjini Goodbless Lema,aliwaambia maelfu ya wananchi ambao walikusanyika katika viwanja vya mahakama hiyo kuwa bado yeye ni jasiri wa hali ya juu sana na kwa hali hiyo atashinda tu
Lema alisema kuwa kitu kilichofanyika katika mahakama hiyo na kisha kutengua ubunge wake kinaonesha wazi jinsi mahakama isivyoweza kutumia demokrasia na hali hiyo kama itaendelea ni wazi kuwa maskini watakosa haki zake za msingi
Lema aliwaambia wananchi wa jimbo lake kuhakikisha kuwa kamwe hawavishiwi roho za uoga kwa kuwa roho hizo za uoga kama zitakuwepo ndani ya jimbo lake ni wazi kuwa wataendelea kuteseka na CCM
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Aikael Mbowe aliwaambia wananchi Jumamosi ndio watajua mbivu na chachu kama watarudia uchaguzi au watakata rufaa
Kutokana na hali hiyo Bw Mbowe alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa watulivu kwa kuwa hata chama hicho bado hakina nguvu ya kupingana na nguvu ya mahakama kwa kuwa mahakama ni muhimili pekee wa nguvu ya Dola.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)