MBUNGE WA SUMBAWANGA MJINI (CCM) AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MBUNGE WA SUMBAWANGA MJINI (CCM) AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA

Hukumu ya kupinga matokeo ya ubunge wa sumbawanga mjini wa Aeshy Hilaly Halphany CCM dhidi ya mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye anadai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.

Madai miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo, mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika. Mahakama imemvua ubunge mbunge wa CCM Bw. Aheshy Hilal. 
Habari zaidi tutawaletea baadae. Kwa hisani ya Mjengwablog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages