
Hapa
ni Mpakani mwa Mikoa ya Rukwa na Katavi kwenye Mlima maarufu wa Lyamba
Lyamfipa. Utawala wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
unaishia hapa, anashusha kibendera kuruhusu Utawala Mpya wa Dkt. Rajab
Mtumwa Rutengwe kupandisha bendera yake tayari kuipepeza
kwenye Milima na Mabonde ya Utawala wake Mpya wa Mkoa Mpya wa Katavi.

Bendera ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya imeshashushwa.

Mkuu
wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akiwa tayari
kupepeza bendera yake kwa mara ya kwanza katika Mkoa wake mpya wa
Katavi baada ya kukabidhiwa Mkoa huo jana.

Safari
ya kuelekea makabidhiano ilianza ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Rukwa
Injinia Stella Manyanya ambaye alianza kwa kumuombea dua Mkuu wa Mkoa
Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Rutegwe mapema kabla ya kuanza safari
kuelekea Wilayani Mpanda Mkoa Mpya wa Katavi ambapo ndipo yalipofanyika
makabidhiano hayo. Mkoa wa Rukwa umegawa na kuundwa Mkoa Mpya wa
Katavi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kusogeza huduma zake kwa
wananchi. Kwa pamoja viongozi wote wa Mikoa ya Rukwa na Katavi
wameishukuru sana Serikali ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuugawa
Mkoa wa Rukwa kwa maslahi ya wananchi wake.

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katikati akiwatambulisha
viongozi wapya wa Mkoa Mpya wa Katavi kwa wananchi wa Mkoa huo jana
kwenye uwanja wa Kashaulili Wilayani Mpanda katika makabidhianao ya
Mkoa huo baada ya uliokuwa Mkoa wa Rukwa kugawanywa ikiwa ni jitihada
za Serikali kusogeza huduma kwa Wananchi wake. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
huo Dkt. Rajab Mtumwa Rutegwe na Katibu Tawala Injinia Emmanuel
Kalobelo.

Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wananchi wa Mkoa
Mpya wa Katavi waliojitokeza kwa wingi kabla ya kuwatambulisha viongozi
wao katika uwanja wa Mpira wa Kashaulili uliopo Wilayani Mpanda.
Aliwaomba wananchi hao kuwapa viongozi wao wapya ushirikiano wa dhati
ili kurahisisha utendaji kazi wao kwa maendeleoa ya Katavi na Ukanda
mzima wa Ziwa Tanganyika.

Mkuu
wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akihutubia wananchi
wake wa Mkoa Mpya wa Katavi mara baada ya kutambulishwa kwao na Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa. Aliwaahidi ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha
Katavi inasonga mbele.Picha na Habari Zimeletwa hapa na Hamza Temba - Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa kwa habari zaidi Kuhusu Mkoa wa Rukwa Bofya Hapa...>>>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)