
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa NEC Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw.Nape Nnauye
akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo ya chama hicho
zilizopo mtaa wa lumumba jijini Dar es salaam, juu ya uchaguzi mdogo
wa ubunge ulifanyika jana katika jimbo la Arumeru mashariki, ambapo
mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari ameibuka mshindi kwa kura 32.972,
chama cha mapinduzi kimekubali matokeo hayo yaliotangawa na Tume ya
uchaguzi leo asubuhi
Nape kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza kijana Nasari na
kusema "Tunampongeza Joshua Nasari na hakuna hujuma yoyote uchaguzi
ulikuwa huru na haki", lakini pia akawapongeza wananchi wa jimbo la
Arumeru kwani hiyo ndiyo Demokrasia yao.

Baandhi
ya wandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo leo
wakimsikiliza Nape Nnauye alipokuwa akiongea nao juu ya uchaguzi
huo.Picha na Philemon Solomon
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)