*Mchezo wageuka Ulingo kama Misri, Wachezaji wamkimbiza mwamuzi kama Kuku uwanjani. Pichani
juu, ni kipa wa Yanga, Shaban Kado, akiokoa moja ya hatari
zilizoelekezwa langoni kwake, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania
Bara kati ya Yanga na Azam, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam leo jioni.
Katika
mchezo huo Azam imeibuka na ushindi wa mabao 3-1, huku Yanga ikicheza
pungufu wakiwa wachezaji 9 uwanjani baada ya wachezaji wawili, Haruna
Niyonzima na Haroub Canavaro kupewa kadi katika kipindi cha kwanza cha
mchezo kufuatia vurugu zilizotokea uwanjani hapo.
Mwamuzi
wa mchezo huo, Israel Mongo, akitoka baruti 'Nduki' kuwakimbia
wachezaji wa Yanga baada ya kutoa kadi mbili kwa wachezaji wa Yanga,
jambo ambalo lilipingwa na wachezaji wa Yanga na kuzua mtafaruku
uwanjani hapo.
Tukio
jingine lililowashangaza mashabiki wa Soka waliokuwapo uwanjani hapo ni
tukio hili la Askari Polisi aliyetinga magwanda, ambaye alitinga
katikati ya uwanja wakati waa vurugu hizo na kuamulia ugomvi, jambo
ambalo lingeweza kuamsha hasira zaidi za mashabiki.Picha Na Sufiani Mafoto








No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)