TAARIFA KWA UMMA
UTANGULIZI
Baada
ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari
nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa
ufafanuzi ufuatao:
1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi
Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii
(social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).
2.
Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi
anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo
ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha
yake.
3.
Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini
lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa
yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.
4.
Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida
ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na
vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa
ziwepo mahospitalini zinakohitajika.
5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.
TAMKO LETU:
JANA
TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO
ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA
MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.
KUTOKANA
NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI
RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS
AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.
PIA
WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI
NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA
TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.
MADAKTARI
TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR.
LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI
NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA
KIUTENDAJI.
SOLIDARITY FOREVER.
RAIS(MAT)





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)